Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mh!!!!!!!!!
 
kifuatilia utagundua katika nchi yoyote duniani,watu wanaokuja toka nchi nyingine au eneo jingine kwa minajili hasa ya biashara wanafanikiwa zaidi kuliko wenyeji wa nchi au eneo hilo.

Nini sababu? Hebu tufuatilie pamoja katika makala hii ambapo nitakupa sababu za msingi zinazowafanya wageni kufanikiwa zaidi kuliko wenyeji wa eneo husika.
 
Kuwa na lengo Moja:
Wahamiaji au wageni wanafanikiwa kubaki na lengo lao kuu na hivyo kufanikiwa kuweka nguvu na msukumo katika lengo kuu ambalo ni kutafuta maisha bora zaidi au kukuza mitaji na biashara zao.
 
Kuwa Mbali na Ndugu na Jamaa Masikini
Ndugu,jamaa na marafiki wanaweza kukupandisha lakini pia kukushusha katika maendeleo yako. Kwahiyo aina gani ya watu unahusiana na kuwa nao karibu wanachangia sana safari yako ya mafanikio au kuanguka kwako. Fanya utafiti kuona una watu wa aina gani wanaokuzunguka na chagua kubaki na wale wenye kukupandisha juu na wenye mawazo chanya.
 
Ukiwa mgeni kwenye nchi au eneo fulani unanafasi kubwa ya kuwaepuka ndugu na jamaa na marafiki hasi wenye kukuvuta nyuma. Hii ni sbabu nyingine inayowafanya wageni kufanikiwa zaidi. Hawana ndufu,marafiki na jamaa wengi wanaowavuta kurudi nyuma.
 
Ukiwa karibu na nyumbani kwenu ambako familia ni kubwa na mahitaji ni makubwa, ni ngumu sana kujikwamua na kwenda mbele sababu kila jicho lenye mahitaji litakuangalia. Ukiwa mbali inapunguza tatizo hilo na mategemeo toka kwa ndugu na jamaa wenye mahitaji na wanaokutegemea uwasaidie yanakuwa chini.
 
Wageni Unajiweka Kwenye Kundi Maalumu
Wageni wanajiweka au wanawekwa na wenyeji katika kundi maalumu,kundi la juu. Hivyo wanatakiwa kuishi katika nafasi hiyo. Wanategemewa wataishi nyumba bora na kufanya kazi nzuri. Ili kubakisa hadhi hiyo ya juu wanatakiwa kujituma zaidi kuliko wale wenye hadhi ya chini.
 
Hata ndani ya nchi utaona watu wanaotokea katika mkoa au mji mmmoja wanasaidiana zaidi katika kupandisha hali zao za maisha. Angalia mfano wa makabila ya Wachaga na Wahaya nchini Tanzania. Kila penye fursa na kuna mtu wa kabila lake atampa kipaumbele yeye kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…