Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Siku ya Leo nataka nikujulishe baadhi ya sifa za mtu anaejielewa.

1. Anafanya mambo kwa wakati
-~Mtu anaejielewa siku zote anaratiba inayomwongoza kufanya mambo yake kwa wakati. Muda ni rasilimali isiyoweza kurudishwa wala hauna spea ukipita ndio basi tena. Kila jambo linawakati maalum wakufanya hakuna jambo lilo hewani tu.
 
2. Anasikikiza kwa makini mwingine anasema nini
~~~Mtu anaejielewa maranyingi sio wa kuropoka tu au kuongea yeye mwenyewe bali huwa tayari kusikiliza mwingine anasema kitu gani bila kujali cheo au ukubwa alionao.
 
5.Anajifunza na kuongeza maarifa kila siku
~~~ Mtu anaejielewa hupenda siku zote kutafuta maarifa hata kwa gharama yoyote ile. Kwa sababu maarifa hujenga maisha kwa sehemu kubwa ya mwanadamu. Kuna msemo wanasema mtu Mzee anayejifunza ni sawa na kijana Bali mtu kijana asiyejifunza ni sawa na Mzee.
 
4. Anakuwa na malengo,mipango inayotekelezeka
~~~Mtu anaejielewa haishi kama ndege au mnyama. Lazima awe na malengo ili kufikia ndoto zake. Malengo ya muda mfupi,ya kati na ya muda mrefu. Je baada ya miaka miwili nitakuwa wapi? Baada ya miaka kumi nitakuwa wapi? Haya ni baadhi ya maswali ambayo hujiuliza.
 
6.Anajiamini kwenye mambo yake
~~~Kujiamini ni uwezo wa kufanya jambo fulani na kulifanikisha. Watu wanaojielewa wanaimani kubwa na yenye nguvu katika kuhakikisha wanatimiza mambo wanayotaka au ndoto zao.
 
8. Anamtambua Muumba wake
~~~Mtu anaejielewa lazima atambue kuwa yupo Mungu anaemuwezesha katika jitihada zake. Siku zote atamuhusisha Mungu katika mambo yake yote anayofanya. Maana Mungu ndio chimbuko la mambo yote huwezi mtenganisha Mungu na mafanikio.
 
9. Yuko tayari kukosolewa
~~~Mtu anaejielewa hukubali kukosolewa kwa sababu anaamini yeye ni mwanadamu hawezi kuwa mkamilifu kwa kila kitu. Hivyo hupenda kujifunza alipokosea kwa kufuata ushauri wa wengine.
 
10.Anapenda kuona wengine wanafanikiwa katika maisha yao.
~~~Mtu anaejielewa hupenda kuona wengine wakiwa vizuri kwenye maisha yao.Yupo tayari kuingia gharama kuhakikisha mtu mwingine anapata kile anachokitaka hata kama hana hujitahidi kutoa ushauri. Kuna msemo unasema ukitaka kufanikiwa kirahisi wasaidie wengine kuwa na maisha bora nawe utafanikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…