Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

HALI YA AFYA YA HAWA NI MBAYA SANA HUKO MHIMBILI : . Kama tunakumbuka Diamond alishawahi kuimba wimbo wa nitarejea na kumshirikisha dada mmoja aliyekuwa na sauti nzuri ya kumtoa nyoka pangoni.Mwanadada huyo aliyekuwa akijulikana kwa jina la Hawa alikuja kupotea ghafla katika tasnia pamoja na kwamba hakukaa kwa muda mrefu katika game. Mwanadada huyo kwa sasa yuko hoi kitandani katika hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na ugonjwa wa ini unaomsumbua kwa muda mrefu sasa. Moja ya wamiliki wa kituo cha kusaidia watumiaji wa madawa ya kulevya ambako Hawa alikuwa akitibiwa, Pili Misana alisema kuwa kwa muda mrefu sasa hawa amekuwa na tatizo la ini ambalo kwa kiasi kikubwa limesababishwa na utumiaji wa muda mrefu wa madawa ya kulevya na unywaji wa pombe kali.hata hivyo pili missana anasema kuwa hali ya hawa ilianza kuimarika kwa sababu alikuwa tayari alishakubali kutoka katika matumizi hayo lakini kumbe alikuwa tayari ameshaanza kuathirika ini. unajua hali ya hawa ilikuwa tayari ilishaanza kutengemeaa,lakini kumbe alikuwa tayari ameshapata tatioz la ini muda mrefu. kutokana na unywaji wa pombe kalikwa sasa hivi hali yake sio nzuri na anaendelea na matibabu katika hospitali ya muhimbili.-Alisema Pili Misana. Ikumbukwe kuwa Hawa alishawahi kuripotiwa na kipindi cha shilawadu siku za nyuma kuwa ameathirika sana na utumiaji wa madawa ya kulevya na wazazi wake kuomba asaidiwe ili arudi katika hali yae ya kawaida.
 
Tunaambiwa Jackie Cliff Patrick anaelekea kumaliza kifungo chake huko China baada ya kubambwa na madawa ya kulevya na kufungwa 2013 huko Macau, China. . Kwa upande wa Sandra Khan maarufu Kama Binti Kiziwi Tunaambiwa uwezekano yeye labda atakuwa amefungwa maisha huko Hong Kong, China. Kamishna wa sheria na kupambana na dawa za kulevya nchini Akimzungumzia Binti Kiziwi, aliyenaswa Hong Kong, Julai 15 mwaka 2013 na madawa ya kulevya aina ya heroin zaidi ya kilo moja na kuhukumiwa wiki hiyohiyo, Kamishna Kakolaki alisema unapokamatwa na madawa ya kulevya kuanzia kilo moja adhabu yake ni kifungo cha maisha au faini ya shilingi bilioni 1.4 (kwa pesa za Kitanzania). . “Hivyo, ili Binti Kiziwi aachiwe gerezani, inabidi atoe kiasi hicho cha fedha aidha kwa kuchangiwa au vyovyote, vinginevyo na kwa sheria za Hong Kong kwa kuwa hakutoa fedha, tayari ameshafungwa maisha. “Kikitolewa kiasi hicho cha fedha anaachiwa huru hata kesho,” alisema Kamishna Kakolaki alipoulizwa na gazeti la Amani GPL . Jackie Cliff Patrick alikuwa katika top 5 Miss Ilala mwaka 2005 na kuingia top 10 ya Miss Tanzania baadaye alitokea kwenye videos za baadhi ya wasanii wa Bongofleva kabla ya kudakwa huko Macau . Sandra Khan yeye alijipatia umaarufu baada ya kuwa model wa wimbo wa Binti Kiziwi wa Z Anto baadaye walioana ndoa ikavunjika baada ya mwaka mmoja. Mwaka 2015 katika interview Z Anto alisema Hana uhakika Kama Binti Kiziwi yupo hai huko China, Z Anto alisema kabla aliwahi kumshtukia Binti Kiziwi kuhusu kujihusisha na dawa za kulevya akamuonya na kuelewa lakini inaonekana hakukoma akaendelea tena mwisho wake ukawa mbaya.
 
Siku sita kabla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, mwanamke mmoja amenusurika kuliwa na mamba wakati akiteka maji kwenye Mto Mgeta, Dakawa mkoani Morogoro, ikiwa ni madhara yanayotokana na kukosekana kwa huduma hiyo muhimu katika kijiji anachoishi.

Martha Malambi (25), baada ya shambulio hilo la Februari 17 lililosababisha kumpoteza mtoto wake wa kiume, Godfrey David (mwaka mmoja na miezi miwili) ambaye alikufa na baadaye maiti yake kusombwa na maji, kwa sasa anaendelea na matibabu katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Hospitali ya Muhimbili (MOI).
 
Ni saa 11:00 jioni katika kijiji cha Ukutu, Kata ya Bwakilachini, Martha akiwa amembeba mwanaye mgongoni, anafika katika Mto Mgeta baada ya kutembea mwendo wa nusu saa akitafuta maji.

“Nilikwenda mtoni kuchota maji nikiwa nimembeba mwanangu, baada ya kujitwisha kichwani wakati naanza kutoka mtoni mamba mkubwa alinivamia kwa nyuma, alinikamata mguu sehemu ya msuli na paja akanivuta mtoni,” anasimulia Martha aliyepambana kijasiri na mamba huyo. Anasema baada ya kudondoka mamba huyo alimvuta mpaka mtoni kwenye kina kirefu kisha kumzamisha chini ya maji, “Nilimhisi mwanangu namna alivyohangaika na maji aliyokuwa anakunywa baada ya sekunde chache alituibua tena juu hapohapo kitenge kikafunguka na mtoto akaondoka na maji, nilipata uchungu mkubwa,” anasema.
 
Anasema mamba alizidi kumbana zaidi na kumvutia bondeni. Wakati wa purukushani hizo alikuwa amembana mguu kwa meno yake na kuacha kiwiliwili, hivyo akawa anapiga kelele kuomba msaada huku akiendelea kupambana naye.

Mama huyo wa watoto wawili, huku mmoja aliyemuacha nyumbani akiwa na umri wa miaka mitano, anasema alitumia nguvu zaidi kupanua mdomo wa mamba ili kumpa maumivu, lakini aliendelea kumshinda nguvu kutokana na urefu wa mnyama huyo kuwa maradufu ya urefu wake.
 
Kutokana na purukushani ile, aliona hajanidhibiti vizuri kwa sababu alinishika mguu mmoja, akajaribu kusogea kwenye kina kifupi cha maji ili anikamate vizuri,” anasimulia Martha.

Anasema hatua ya mamba huyo kusogea kwenye kina kifupi cha maji ya mto kutoka kina kirefu, kilimsaidia kuyafikia matete (magugu maji) hivyo aliyashika na kuyang’ang’ania kwa nguvu huku akiomba msaada kwa kupiga kelele.
 
Mwanamke huyo anasema ilikuwa bahati kwake, kwani kulikuwa na wavulana ambao hawakuwa mbali na mto huo ambao walisikia kelele za kuomba msaada na kuwahi eneo hilo, wawili wakiwa na magongo wawili wengine mapanga hivyo kuingia kwenye maji na kuanza kumshambulia mamba huyo.

Pamoja na msaada huo wa watu, mamba aliendelea kung’ang’ania mguu wake lakini mashambulizi yalivyozidi mamba alionekana kuchoka na kupata maumivu, hivyo kuuachia mguu na kuzama majini.
 
Hata hivyo, Martha anasema kabla hajaokolewa alikata tamaa kwani alihisi tayari amekufa: “Yule mamba mkubwa karibu mara mbili ya mwili wangu aliniogopesha sana, sikuwa nimewahi kumuona kwa macho yangu kabla ya siku hiyo. Viboko nawajua vizuri kwa sababu nimewahi kuwaona mara nyingi kijijini.
 
Wale vijana walinichukua na kunipeleka nchi kavu baadaye Zahanati ya Lukumi, ambako walinipatia huduma usiku kucha, asubuhi ya Februari 18 walinisafisha vizuri maeneo yote yaliyoathiriwa na kucha na meno ya mamba huyo.”
 
Anasema kutokana na ukubwa wa majeraha hayo na mguu kuvunjika, alihamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako baada ya kuhudumiwa takriban siku tano walimweleza kuwa tatizo lake inabidi apelekwe Muhimbili. Safari yake kwenda MOI ilianza akiwa yeye na wauguzi tu, alipofika alipokelewa na kupelekwa chumba cha upasuaji ambako alirekebishwa maeneo ya nyonga ambayo pia yaliathiriwa.
 
Nimefika MOI nikiwa peke yangu. Sina ndugu hapa Dar es Salaam wala ndugu yeyote kutoka nyumbani ambaye amefika hospitali tangu siku hiyo. Nashukuru wauguzi na madaktari wamekuwa wakinisaidia wakati wote, ninapata matibabu vizuri, ninapata chakula, nashukuru kwa hilo” anasema na kusisitiza kuwa familia yake ni maskini, hivyo hana mawasiliano nao kwani simu aliyoitegemea ilisombwa na maji.
 
Uhaba wa maji Ukutu

Martha anayeishi na wazazi wake kijijini hapo, anasema hawawezi kuepuka kufuata maji mtoni kwa kuwa hakuna chanzo kingine cha maji kijijini zaidi ya mto Mgeta, miaka yote wamekuwa wakichota maji hapo
 
Back
Top Bottom