Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkoa wa Shinyanga ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye msimbo wa posta 37000[1]. Mkoa umepakana upande wa kaskazini na mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera, upande wa kusini na Mkoa wa Tabora. Mkoa wa Kigoma uko upande wa magharibi, na mkoa wa Simiyu upande wa mashariki.

Makao makuu yako mjini Shinyanga.
 
Kabla ya kumegwa upande wa mashariki na kuzaa mkoa wa Simiyu Shinyanga ilikuwa na wakazi 2,796,630 kufuatana na sensa ya mwaka 2002. [1].

Maeneo yanayobaki yalihesabiwa kuwa na wakazi 1,534,808 katika sensa ya mwaka 2012.[2]
 
Mkoa wa Shinyanga una wilaya 5: Kahama mjini, Kahama Vijijini, Kishapu, wilaya ya Shinyanga vijijini na wilaya ya Shinyanga mjini.

Wilaya tano zimepelekwa kwenda mikoa mipya ya Simiyu na Geita
 
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Kahama Mjini : mbunge ni Jumanne Kishimba (CCM)
Kishapu : mbunge ni Suleiman Nchambi (CCM)
Msalala : mbunge ni Ezekiel Maige (CCM)
Shinyanga Mjini : mbunge ni Steven Masele (CCM)
Solwa : mbunge ni Ahmed Ally Salum (CCM)
Ushetu : mbunge ni Elias Kwandikwa (CCM)
 
Mkoa wa Manyara ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 27000[1] . Umepakana na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa mashariki, Mkoa wa Dodoma upande wa kusini na mikoa ya Singida na Shinyanga upande wa magharibi.
 
Mkoa wa Manyara umetengwa na Mkoa wa Arusha mwaka 2002 kwa azimio la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa na eneo la km² 46,359.

Babati ndiyo makao makuu ya mkoa.
 
Wakazi

Jumla ya wakazi mkoani ilikuwa 1,425,131 katika sensa ya mwaka 2012. Idadi hiyo imepatikana katika wilaya zifuatazo (idadi ya wakazi katika mabano mwaka 2002): Babati (303,013), Hanang (205,133), Mbulu (237,882), Simanjiro (141,676) na Kiteto (152,757)
 
Sensa zinaonyesha kwamba ni kati ya mikoa ya Tanzania yenye ongezeko kubwa la wakazi. Pia ni kati ya mikoa yenye maambukizi machache zaidi ya Ukimwi.

Wenyeji wa mkoa huu ni pamoja na Wairaqw, Wamasai, Wasonjo, Wafyomi na Wabarbaig wakijihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji kama njia ya kuingiza kipato chao cha kila siku.
 
Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi 7 yafuatayo:

Babati Mjini : mbunge ni Pauline Gekuli (Chadema)
Babati Vijijini : mbunge ni Jitu Vrajilal Soni (CCM)
Hanang’ : mbunge ni Mary Nagu (CCM)
Kiteto : mbunge ni Emmanuel Papiani (CCM)
Mbulu Mjini : mbunge ni Zacharia Paulo Issaay (CCM)
Mbulu Vijijini : mbunge ni Flatei Massay (CCM)
Simanjiro : mbunge ni James Kinyasi Ole Millya (Chadema)
 
5b1e29f8524c1e13312be62792498150.jpg
 
Umepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani,i kufuatana na mwendo wa saa, ni: Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga na Mara.

Wilaya zake ni Monduli, Longido, Meru, Arusha Vijijini, Arusha Mjini,Ngorongoro na Karatu.

Makao makuu yapo Arusha mjini.
 
Eneo lake ni km za mraba 86,100 zikiwemo km² 2,460 za maji ya ndani.

Kati ya milima yake Oldoinyo Lengai (2,878 m) bado ni volkeno hai, na mlima Meru ni volkeno iliyolala tangu mwaka 1910.
 
Mvua hunyesha kati ya milimita 1,800 kwa mwaka mlimani Arusha hadi mm 508 kwa mwaka katika maeneo makavu.

Mkoa wa Arusha ndio kitovu cha utalii Tanzania Bara. Kuna mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori Ngorongoro, Serengeti, Olduvai, Arusha, na Ziwa Manyara. Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Tarangire ziko karibu
 
Barabara ya lami Dar es Salaam-Nairobi inavuka eneo lake. Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro wahudumia miji ya Arusha na Moshi.

Arusha hulimwa kahawa, nafaka, pareto, katani, pamba, alizeti.
 
Fosfati inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea.

Kati ya wakazi asili wa mkoa ndio Waarusha, Wameru, Wairaqw na Wamasai.
 
Back
Top Bottom