Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

6555A4F4-940A-4F31-B8FC-09702F12EB98.jpeg
 
Hifadhi hiyo ni ndogo (ina ukubwa wa kilometa za mraba 542 tu) lakini ina mandhari yenye maeneo matatu tofauti.

1. Katika magharibi, kreta ya mlima Meru inafanya Mto wa Jekukumia, kilele cha Mlima Meru kwa juu ni cha mviringo. Unafanya hifadhi kuwa na mazingira ya baridi.
 
2. Kreta ya Ngurdoto Kusini-Mashariki ni yenye uoto wa nyasi.

3. Maziwa yenye kina, Mamaella Kaskazini-Mashariki yana rangi tofauti za algali na hujulikana kwa kuwa na ndege wenye midomo mirefu wanaoishi pembezoni mwa maziwa (sehemu zenye matope).
 
Hifadhi hii ni maarufu kwa wanyama jamii ya tumbili wajulikanao kama mbega weusi na weupe.

Wanyama wengine wanaopatikana kwa wingi katika hifadhi hii ni pamoja na twiga, pundamilia, nyati na digidigi.
 
Aidha unaweza kuwaona chui wakibarizi katika vivuli vya matawi ya miti inayokingwa na maanguko ya maji huku makundi kadhaa ya batamaji yakitafuta wadudu katika maziwa ya Momella.

Zaidi ya aina 400 za ndege wamethibitika kupatikana ndani ya hifadhi hii.
 
Safari ya miguu kupanda mlima Meru ni moja ya burudani muhimu katika hifadhi hii: mpandaji anahitaji siku 3-4 kupanda mlima.

Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ni kati ya mwezi Juni na Februari ingawa mvua inaweza kunyesha mwezi Novemba.
 
Hifadhi ya Ruaha iko katikati ya Tanzania umbali wa kilometa 128 magharibi ya mji wa Iringa. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 1300.

Hifadhi hii ni maarufu kwa wanyama aina ya kudu wakubwa na wadogoambao hupatikana kwa wingi katika hifadhi. Ustawi wa hifadhi hii hutegemea kwa kiasi kukubwa
 
Aina mbalimbali za samaki , viboko, na mamba hupatikana kwa wingi katika mto huu. Wanyama kama pofu na swala pala hunywa maji katika mto Ruaha ambao ni mawindo ya kudumu kwa wanyama wakali kama simba, chui, mbweha, fisi na mbwa mwitu.
 
Hifadhi hii inao idadi kubwa ya tembo wanaokusanyika katika eneo moja kuliko eneo lingine lolote Africa Mashariki.
Hifadhi hii ina sifa ya kuwa na wanyama na mimea karibu yote inayopatikana katika sini na Mashariki mwa Africa.
 
Safari kwa kutumia ndege za kukodi kutoka Dar es Salaam, Arusha, Iringa na Mbeya.Pia kwa njia ya barabara.

Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii na kuangalia wanyama wakubwa ni wakati wa kiangazi, kati ya mwezi Mei hadi Desemba. Kuangalia ndege na mauawakati wa masika(Januari hadi Aprili)
 
Milima ya Udzungwa ni jina la hifadhi inayopatikana katika bara la Afrika, nchini Tanzania, mkoani Morogoro, wilaya ya Kilombero.

Hifadhi iko umbali wa kilometa 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilometa 65 kutoka katika Hifadhi ya Mikumi.
 
Jina la hifadhi limetokana na milima hiyo ya Udzungwa (yaani nchi ya Wadzungwa, tawi la Wahehe).

Ina ukubwa wa kilometa mraba 1990, na ni hifadhi yenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambao hawapatikani katika sehemu nyingine yoyote duniani.
 
Jina la hifadhi limetokana na milima hiyo ya Udzungwa (yaani nchi ya Wadzungwa, tawi la Wahehe).

Ina ukubwa wa kilometa mraba 1990, na ni hifadhi yenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambao hawapatikani katika sehemu nyingine yoyote duniani.
 
Kati ya aina kumi na moja za jamii ya nyani wanaopatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katika hifadhi hii pekee ambao ni: "Mbega Mwekundu wa Iringa" (Iringa red colobus monkey) na "Sanje Crested mangabey" ambaye alikuwa hajulikani mpaka mwaka 1979. Kuna aina nyingine nne za ndege ambao hawakufanyiwa uchunguzi ambao ni: chozi bawa jekundu (rufous-winged sunbrid) na jamii mpya iliyogunduliwa ya aina ya kwale wa Udzungwa zinazofanya hifadhi hii kuwa ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege pori barani Afrika.
 
Back
Top Bottom