Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Arumeru Magharibi : mbunge ni Gibson Ole Mesiyeki (Chadema)
Arumeru Mashariki : mbunge ni Joshua Nassari (Chadema)
Arusha Mjini :mbunge ni Godbless Lema (Chadema)
Karatu : mbunge ni Wille Qulwi Qambalo (Chadema)
Longido : mbunge ni Onesmo Ole Nangole (Chadema)
Monduli : mbunge ni Kalanga Julius Laizer (Chadema)
Ngorongoro : mbunge ni William Tate ole Nasha (CCM)
 
Wilaya ya Monduli ni kati ya wilaya tano za Mkoa wa Arusha yenye postikodi 23400 [1]. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Monduli ilihesabiwa kuwa 158,929.
 
Wilaya hii iko katika kaskazini mashariki ya Tanzania. Imepakana na Kenya upande wa kaskazini, Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Arusha Vijijini upande wa mashariki, Mkoa wa Manyara upande wa Kusini na Wilaya ya Ngorongoro pamoja na Wilaya ya Karatu upande wa magharibi.
 
Wilaya ya Monduli ilikuwa sawa na Jimbo la Uchaguzi la Monduli wakati wa uchaguzi wa bunge. Eneo limegawiwa kwa kata 15 na 51 vijiji au mitaa ya mjini. Eneo lote ni kilomita za mraba 6,419.

Makao makuu ya wilaya iko Monduli Mjini ambayo ni moja wa miji midogo miwili (pamoja na Namanga) katika wilaya yenye tabia ya vijijini.
 
Mlima Meru ni mlima wa volkeno wenye urefu wa mita 4565 (futi 15064) juu ya usawa wa bahari. Mlima huo ni wa tano kwa urefu katika bara la Afrika.

Mlima Meru unapatikana ndani ya Hifadhi ya Arusha ambayo ilianzishwa mwaka 1960 na ambapo wanyamapori kuzunguka Maziwa ya Momella na volkeno ya Ngurudoto (Ngurudoto crater) walihifadhiwa na kulindwa katika eneo hili.
 
Mlima Meru ni mlima wa volkeno wenye urefu wa mita 4565 (futi 15064) juu ya usawa wa bahari. Mlima huo ni wa tano kwa urefu katika bara la Afrika.

Mlima Meru unapatikana ndani ya Hifadhi ya Arusha ambayo ilianzishwa mwaka 1960 na ambapo wanyamapori kuzunguka Maziwa ya Momella na volkeno ya Ngurudoto (Ngurudoto crater) walihifadhiwa na kulindwa katika eneo hili.
 
Vivutio katika hifadhi hiyo vinajumuisha volkeno, maziwa, misitu na wanyamapori kama twiga, tembo, pundamilia, nyati na wengine wengi. Pia kuna ndege wa aina nyingi wakiwemo flamingo, na misitu katika mlima Meru ni makazi ya nyani.

Kupanda Mlima Meru kunachukua siku tatu hadi nne na wakati mzuri kwa kupanda mlima ni kuanzia mwezi Juni hadi Februari ambapo mvua zinaweza kunyesha katika mwezi Novemba. Na wakati mzuri wa kuona mlima Kilimanjaro kutokea Meru ni kati ya Desemba na Februari.
 
323D8474-6A82-4D3A-A676-E50F5AF3C69B.jpeg
 
Hifadhi ya Taifa ya Arusha yenye Mlima Meru, wenye volkano maarufu na mwinuko wa m. 4566 (futi 14990), inapatikana katika Mkoa wa Arusha, Kaskazini Mashariki mwa Tanzania, umbali wa kilometa 32 kutoka mji wa kitalii wa Arusha.
 
Hifadhi hiyo ni ndogo (ina ukubwa wa kilometa za mraba 542 tu) lakini ina mandhari yenye maeneo matatu tofauti.

1. Katika magharibi, kreta ya mlima Meru inafanya Mto wa Jekukumia, kilele cha Mlima Meru kwa juu ni cha mviringo. Unafanya hifadhi kuwa na mazingira ya baridi.
 
Back
Top Bottom