Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Saratani ya Ovari : Kuvimbiwa mara kwa mara inaweza kuwa dalili

Ni theluthi moja tu ya wanawake wanaomuona daktari licha ya kuwa na dalili kubwa, wasema utafiti shirika la kupambana saratani ya Ovari-Target Ovarian Cancer.

Unapokabiliwa na kuvimbiwa, 34% ya wanawake 1,142 waliohojiwa na kampuni ya YouGov ndio waliosema wanaweza kumuona daktari.
 
Nusu walisema hatua ambayo wanaichukua ni kubadili lishe yao kwa kufanya vitu kama kula vyakula vyenye chachu kama maziwa ya mgando ama Yogati

Shirika hilo la kupambana na saratani ya Ovari linafofia kile linachosema ni "viwango vidogo vya uelewa " wa kuvimbiwa kama dalili ya saratani.
 
Utafiti wa awali uliofanywa na shirika hilo ulionyesha kuwa ni mwanamke mmoja tu kati ya watano anayeweza kung'amua kuwa kuvimbiwa ni dalili ya saratani.

Utafiti huu unazungumzia kuhusu wanawake wote wa Uingereza na waliulizwa ni nini wangekifanya iwapo ''wangekua na tatizo la kuvimbiwa kwa mara kwa mara''

Wengi hawakuweza kusema kuwa wanaweza kumuona daktari kutokana na tatizo hilo.
 
Back
Top Bottom