Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Haya Ndiyo Mambo Makubwa Mawili, Ambayo Ni Lazima Ukutane Nayo Sana Kwenye Safari Ya Mafaniko Yako.
Katika safari yako ya mafanikio, yapo mambo makubwa mawili ambayo ni lazima ukutane nayo sana. Mambo haya kila binadamu anakutana nayo sana, hakuna mtu ambaye hakutani nayo hata kama hutaki mafanikio, utakutana nayo tu.
 
Hata kwa kila iitwapo leo, mambo haya pia utakutana nayo pia. Hakuna siku ambayo itapita bila kukutana na mambo haya mawili iwe kwa kidogo au sana utakutana nayo tu utake, usitake lakini uwe na uhakika utakutana nayo.
 
Mambo hayo ambayo kila mtu anakutana nayo kwenye safari ya mafanikio ni fursa na changamoto. Kila mtu, kila siku anakutana na fursa na changamoto kwenye maisha yake. Hata leo ni lazima pia utakutana na mambo haya makubwa mawili.
 
kama nilivyosema, kitu cha kwanza ni fursa, kila kukicha zipo fursa ambazo utakutana nazo. Fursa hizi zinaweza zikawa zinaonekana kwa wazi au hazionekani kwa wazi. Hakuna haja ya kusema kwamba mbona mimi fursa hizo sizioni, sio kweli.
 
Kile kitendo cha kuamka tu na kukutana na watu na mkabadilishana mawazo, hiyo ni fursa kubwa sana kwako kwa siku. Kupitia watu hao mtabadilishana mawazo na wewe unaweza ukatapa kitu cha kuweza kukusaidia kwenye maisha yako
 
Ikiwa lakini upo upo tu, unakutana na watu kazi yako nikupiga majungu na kujifanya wewe ndio mwongeaji sana, sahau hizo fursa kuweza kuziona. Utapotea sana na utabaki kila siku kulaumu kwamba dunia ngumu kwako kumbe sio kweli.
 
Kipi unachokiona kila kunapokucha? Unaona unazungukwa na fursa au unaona kila kitu unazungukwa na hasi nyingi ambazo haziwezi kukusaidia wewe maishani mwako. Unatakiwa kujifunza kutambua fursa za mafanikio yako kila siku.
 
Kitu cha pili ni changamoto, bila kujali unakutana na changamoto za ukubwa upi, lakini kila kukicha unakutana na changamoto. Na kupitia changamoto hizo ndizo zinatupaisha na kutufikisha kwenye mafanikio makubwa ikiwa utazitatua kwa kiasi kikubwa.
 
31604bab99ccfb64c60388a46216a00c.jpg
Hamna kitu hapo sekta nyeti
 
Wapi ulipo, na wapi maisha yako yapo, hiyo haijalishi. Kikubwa tatua changamoto zinazokuzunguka na utaweza kufanikiwa. Huwezi kukwepa changamoto hata kidogo, changamoto za kimaisha zipo na ni lazzima ukutane nazo.
 
Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo makubwa mawili ambayo ni lazima uweze kukutana nayo sana kwenye maisha yako na kila siku. Jiandae kukutana na mambo hayo na ili yawe kwa faida kubwa kwako na ya kukufanikisha.
 
1. Anayetaka usawa sana mwisho wake hugeuka mchawi.
Katika hekima hii ya maisha na mafanikio ina maana kwamba, tukiwa sisi kama binadamu tukubali kuwa binadamu kutofautiana kupo. Siyo kwa sababu fulani kapata baiskeli ni lazima na wewe upate au fulani kapata nyumba na wewe unawaza lazima nami nipate kwa njia yoyote hata isiyo ya halali.
 
Maneno kama haya mwishowe humsukuma mtu kutumia hila mbaya au njia zisizo za kawaida kama vile uchawi au kila aina ya dhuluma aijuae yeye ili kumwezesha kupata mafanikio hayo. Hekima hii hutumika sana katika kuwaonya wanaopenda kujikweza na kujiona wao ni wao kwamba kila kitu lazima wapate kama wanavyowaona wengine.
 
Watu hao wanasahau kuwa si kila kitu mnaweza kuwa sawa. kujaribu kuwa sawa na watu wengine kwa kila kitu huko ni sawa na kutafuta kwako wewe kuweza kujiumiza. Kwa kuliona hili, hekima za maisha na mafanikio zimeweka wazi, ukitaka usawa mwisho wake hugeuka kuwa uchawi na huo ndio ukweli halisi hata kama unauma.
 
2. Mwenda usiku amesifiwa kulipokucha.
Kuna wakati unaweza ukawa unatenda jambo la aina fulani ambalo jambo hilo watu wengine wanakuwa hawalijui kabisa. Mtu huyu anayetenda jambo lisiilofamika katika hekima anafananishwa na mtu mwenda usiku au mtu yule anayetembea usiku asijue ni nini kilichopo mbele yake ilimradi tu anaenda.
 
Kwa kawaida mtu huyu anayetembea usiku au anayetenda jambo ambalo kwa wakati ule wengine hawalielewi na inapotokea jambo hilo linapoonyesha mafanikio ndipo watu wanaanza kumsifu. Hekima hii hutumika sana kwa mtu anayechekwa na wenziwe juu ya jambo alitendalo iwapo wakati ule wale wamchekao hawaelewi usahihi wa lile alitendalo.
 
Si busara na si uungwana kuanza kumcheka mtu kwa kitu usichokijua hata kidogo na wakati mwenzio anakifanya. Kama ni kufanya mwache afanye, lakini ukiendelea kucheka yakitoka mafanikio jiandae kumsifia. Wapo watu ambao wanaonekana mashujaa baada ya kubezwa sana, ndio maana hekima zinatufundisha mwenda usiku amesifiwa kulipokucha.
 
Back
Top Bottom