Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katika mradi wa kishujaa, kikosi cha Brenner kilimpasua mnyoo kuwa maelfu ya sehemu nyembamba zaidi na kupiga picha kila sehemu ya chini ya hadubini meme, kisha kwa kutazama akalinganisha fumwele kutoka sehemu moja na sehemu nyingi, ili kuonyesha kila neuroni na sinapsi katika mwili mzima.[18] Hakuna kinachokaribia ngazi hii ya utondoti kuhusu viumbe wengine wowote, na ujumbe huo umetumika kuwezesha tafiti kadhaa ambayo haingewezekana bila utafiti huo.
 
Bongo za wauti zimeundwa kwa tishu laini sana, ikiwa na na texture ambao imelinganishwa na Jell-O.[19] Tishu ya ubongo hai ni ya rangi waridi kwa nje na nyeupe kwa wingi ndani, huku kukia na mabadiliko utofauti mdogo wa rangi. Bongo za wauti zimezungukwa kwa mfumo wa tandu za tishu unganishi ziitwazo meninji zinazo tofautisha fuvu na ubongo.[20] Kifuniko hiki chenye safu tatu kinajumuisha (kutoka nje) dura mama ("mama mgumu"), mama araknoida ("mama mwembamba"), na mama pia ("mama laini ").
 
Araknoida na pia zimeshikana kimaumbo na hivyo huchukuliwa kuwa safu moja, ya pia-araknoida. Chini ya araknoida kuna nafasi ya araknoida ndogo ambayo ina ugiligili wa ubongo na uti wa mgongo (CSF), ambayo huzunguka katika nafasi nyembamba kati ya chembechembe na penyu ziitwazo ventrikali, jukumu lake ni kurutubisha, kukimu, na kulinda tishu za ubongo.
 
Mishipa ya damu huingia mfumo mkuu wa neva kupitia nafasi isiyo na mishipa juu ya mama pia. Chembe katika kuta za mishipa ya damu zimeshikana kwa nguvu sana, na hivyo kuunda mpaka wa damu na ubongo ambayo huilinda ubongo dhidi ya sumu inayoweza kuingia kupitia damu.
 
wauti wa kwanza walionekana zaidi ya miaka milioni 500 iliyopita (mmi ), katika kipindi cha Kambri, na huenda walifanana kwa kiasi fulani na umbo la kisasa la samaki balika (hagfish).[21] Papa walionekana takribani miaka milioni 450 iliyopita, amfibia yapata miaka milioni 400 iliyopita, reptilia yapata miaka milioni 350 iliyopita, na mamalia yapata miaka milioni 200 iliyopita.
 
wauti wa kwanza walionekana zaidi ya miaka milioni 500 iliyopita (mmi ), katika kipindi cha Kambri, na huenda walifanana kwa kiasi fulani na umbo la kisasa la samaki balika (hagfish).[21] Papa walionekana takribani miaka milioni 450 iliyopita, amfibia yapata miaka milioni 400 iliyopita, reptilia yapata miaka milioni 350 iliyopita, na mamalia yapata miaka milioni 200 iliyopita.
 
Hakuna spishi ya kisasa inayoweza kuelezewa kuwa "isiyositawi" zaidi ikilinganishwa na nyingine, kwa kuwa zote zina historia ndefu ya mageuko, lakini bongo za samaki balika wa kisasa, mikunga, papa, amfibia, reptilia na mamalia huonyesha tofauti katika ukubwa na uchangamani ambayo kwa kiasi fulani hufuata utaratibu wa mageuko.[22] Bongo hizo zote zina mkusanyiko sawa wa vipengele muhimu vya kianatomia, lakini nyingi hazijakamilika katika balika, ambapo katika mamalia sehemu za kwanza kabisa zimesitawika na kupanuka sana.
 
Bongo zote za wauti huwa na umbo moja la kimsingi, ambayo inaweza kuelewekwa kwa urahisi zaidi kwa kuchunguza jinsi zilivyokua.[23] Dalili ya kwanza ya mfumo wa neva hujitokeza kama utepe mwembamba wa tishu unaoonekana katika mgongo wa kiinitete. Utepe huo hunenepa na kisha kujikunja kuunda neli tupu. Upande wa mbele wa neli hiyo hukua kuwa ubongo. Katika muumdo wake wa kwanza,
 
ubongo huonekana kama vivimbe vitatu, ambayo hatimaye huwa ubongombele, ubongokati, na ubongonyuma. Katika aina nyingi za wauti sehemu hizi tatu hubakia sawa kwa ukubwa katika mnyama mzima, lakini katika mamalia ubongombele hukua kubwa zaidi kuliko sehemu nyingine, na ubongokati mdogo kabisa.
 
Uhusiano kati ya ukubwa wa ubongo, ukubwa wa mwili na vipengee vingine vya kubadilika vimetafitiwa miongoni mwa aina mbalimbali za wauti. Ukubwa wa ubongo huongezeka na ongezeko la ukubwa wa mwili lakini si Proportionellt sett. Ikifanyiwa wastani katika aina zote za mamalia, inafuata sheria nguvu, ikiwa na kipeo husisho cha takribani 0.75.
 
Fomyula hii inatumika katika bongo wastani ya mamalia lakini kila jamii hujitofautisha kutokana nayo, kuonyesha tabia zao changamno.[25] Kwa mfano, jamii ya nyani ina bongo zilizo mara 5-10 kubwa zaidi ya jinsi fomyula inavyotabiri. Wanyama wa kuwinda aghalabu huwa na bongo kubwa.
 
Wakati ubongo wa mamalia unapoongezeka kwa ukubwa, si sehemu zote zinazoongezeka kwa kiwango sawa. Kadri ubongo wa spishi unavyokuwa mkubwa, ndivyo gamba la ubongo linavyokuwa na jukumu kubwa
 
Wana-anatomia wa neva kawaida huchukulia ubongo kuwa na sehemu sita kuu: gamba-nje la ubongo (vizio vya ubongo), gamba-ndani la ubongo (thelamasi na haipothelamasi), gamba-kati la ubongo (ubongokati), ubongonyuma, ponsi, na medula oblongata.[27] Kila moja ya sehemu hizi vilevile zina muundo changamani ndani. Baadhi ya sehemu, kama vile gamba na ubongonyuma, huwa na safu,
 
zilizokunjwa au zilizoviringishwa kutoshea katika nafasi iliyopo. Sehemu zingine huwa na mikusanyiko ya viini vingi vidogo. Ikiwa utofautishaji wa kina ungefanywa kwa msingi wa muundo wa neva, kemia, na miunganiko, maelfu ya maeneo tofauti yanaweza kutambuliwa ndani ya ubongo wa wauti.
 
Baadhi ya matawi ya mageuzi ya wauti yameleta mabadiliko makubwa katika sura za ubongo, hasa katika ubongombele. Ubongo wa papa unaonyesha sehemu za kimsingi katika njia ya moja kwa moja, lakini katika samaki wenye mifupa (wengi wa kisana ni wa aina hii), ubongombele "umepiduliwa", kama soksi imepinduliwa ndani nje.
 
Katika ndege, pia kuna mabadiliko makubwa katika umbo.[28] Moja ya miundo mikuu katika ubongombele wa nedege, kigongo cha ventrikali ya nyuma, kwa muda mrefu kilidhaniwa kulingana na ganglia ya msingi kwa wanyama, lakini sasa inadhaniwa kulingana na zaidi na gamba la nje.[
 
Sehemu kadhaa za ubongo zimehifadhiwa maumbo zao katika aina zote za wauti, kutoka kwa balika hadi kwa binadamu.[1] Hii ni orodha ya baadhi ya sehemu muhimu, pamoja na maelezo mafupi sana ya kazi zao jinsi inavyoeleweka sasa (lakini kumbuka kuwa kazi za nyingi yazo bado zina utata kwa kiasi fulani):
 
Back
Top Bottom