Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Haipothelamasi ni eneo dogo katika shina la ubongombele, ambao uchangamani na umuhimu wake haulingani na ukubwa wake. Inajumuisha viini vingi vidogo, kila mmoja ikiwa na viunganisha tofauti na nyurokemia tofauti. Haipothelamasi ndio kituo kuu cha kudhibiti mzunguko wa usingizi/kuamka, udhibiti wa kula na kunywa, udhibiti wa kutolewa kwa homoni, na majukumu mengine mengi muhimu ya kibayolojia
 
Sawa na haipothelamasi, thelamasi ni mkusanyiko wa viini vilivyo na kazi mbalimbali. Baadhi yavyo vinahusika katika kupitisha habari kutoka na kuelekea vizio vya ubongo. Vingine vinashiriki katika kutia motisha. Eneo lilo chini ya thelamasi (zona insarta) inaonekana kuwa na mifumo ya kuzalisha utendaji wa aina mbalimbali za tabia "kamilishi", ikiwa ni pamoja na kula, kunywa, kunya, na kujamiiana.
 
Sawa na haipothelamasi, thelamasi ni mkusanyiko wa viini vilivyo na kazi mbalimbali. Baadhi yavyo vinahusika katika kupitisha habari kutoka na kuelekea vizio vya ubongo. Vingine vinashiriki katika kutia motisha. Eneo lilo chini ya thelamasi (zona insarta) inaonekana kuwa na mifumo ya kuzalisha utendaji wa aina mbalimbali za tabia "kamilishi", ikiwa ni pamoja na kula, kunywa, kunya, na kujamiiana.
 
Ubongonyuma unadhibiti utendaji wa mifumo mingine ya ubongo ili kuzifanya sahihi zaidi. Kuondolewa kwa ubongonyuma hakumzuii mnyama kufanya kitu chochote hasa, lakini hufanya matendo kuchelewa na isiyo elekevu. Usahihi huu si wa kuzaliwa, bali ni wa kujifunza kwa majaribio na makosa. Kujifunza jinsi ya kuendesha baiskeli ni mfano wa aina ya unyumbufu wa neva unaoweza kufanyika kwa kiasi kikubwa ndani ya ubongonyuma.[
 
Tektama, mara nyingi huitwa "ganda la uonaji", unaruhusu vitendo kuelekezwa katika meneo hewani. Katika mamalia inaitwa "kolikyulasi kuu", na kazi yake iliyotafitiwa sana ni kuelekeza mielekeo ya macho. Pia anaongoza mielekeo ya kufikia vitu pia. Hupoke vichangamshi vikuu vya kuonekana, pia hupokea vichangamshi kutoka katika hisi nyigine ambayo ni muhimu katika kuongoza vitendo, kama vile vichangamshi vya kusikia katika bundi, vichangamshi kutoka katika viungo vya kutambua joto katika nyoka, n.k katika baadhi ya samaki, kama vile mkunga, ndio sehemu kubwa ya ubongo.
 
Paliamu ni safu ya dutu kijivu unao kaa juu ya ubongombele. Katika reptilia na mamalia inaitwa gamba. Paliamu hushiriki katika kazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na unusaji na kumbukumbu ya anga. Katika mamalia, inapo anza kutawala ubongo, hujumuisha majukumu kutoka katika maeneo yaliyo chini ya gamba la ubongo
 
Hipokampasi, kwa hakika, inapatikana kwa mamalia tu. Hata hivyo, sehemu ambapo inatoka, paliamu ya kati, ipo katika wauti wote. Kuna ushahidi kwamba sehemu hii ya ubongo hushiriki katika kumbukumbu za masuala yasiyoshikika na uongozaji katika samaki, ndege, reptilia, na mamalia.[
 
Ganglia ya chini ni kundi la viungo vinayoshikana katika ubongombele, ambavyo uelewa wetu kuvihusu umeongezeka pakubwa sana zaidi katika miaka michache iliyopita. Jukumu la msingi ganglia ya chini inaonekana kuwa uteuzi wa vitendo. Ganglia ya chini hutuma onyo zuizi kwa sehemu zote za ubongo zinazoweza kuanzisha utendaji, na katika hali ya nzuri inaweza kuzuia tendo lenyewe, hivyi kwamba mifumo ya kuanzisha utendaji viweze kushughulikia majukumu mengine. Utuzaji na adhabu hutekeleza zaidi athari zao muhimu katika neva ndani ganglia ya chini.[
 
Kivimbe cha unusaji ni kiungo maalum kinachochakata hisia kutoka katika hisi za unusaji, na kuelekeza matokeo yake katka sehemu ya paliamu inayohusika na hisi harufu. Ni sehemu kubwa ya ubongo katika wauti wengi, lakini imepunguzwa sana katika jamii ya nyani
 
Back
Top Bottom