Hakuna spishi ya kisasa inayoweza kuelezewa kuwa "isiyositawi" zaidi ikilinganishwa na nyingine, kwa kuwa zote zina historia ndefu ya mageuko, lakini bongo za samaki balika wa kisasa, mikunga, papa, amfibia, reptilia na mamalia huonyesha tofauti katika ukubwa na uchangamani ambayo kwa kiasi fulani hufuata utaratibu wa mageuko.[22] Bongo hizo zote zina mkusanyiko sawa wa vipengele muhimu vya kianatomia, lakini nyingi hazijakamilika katika balika, ambapo katika mamalia sehemu za kwanza kabisa zimesitawika na kupanuka sana.