Tektama, mara nyingi huitwa "ganda la uonaji", unaruhusu vitendo kuelekezwa katika meneo hewani. Katika mamalia inaitwa "kolikyulasi kuu", na kazi yake iliyotafitiwa sana ni kuelekeza mielekeo ya macho. Pia anaongoza mielekeo ya kufikia vitu pia. Hupoke vichangamshi vikuu vya kuonekana, pia hupokea vichangamshi kutoka katika hisi nyigine ambayo ni muhimu katika kuongoza vitendo, kama vile vichangamshi vya kusikia katika bundi, vichangamshi kutoka katika viungo vya kutambua joto katika nyoka, n.k katika baadhi ya samaki, kama vile mkunga, ndio sehemu kubwa ya ubongo.