Twiga ni mnyama aishie porini ambaye ndio mrefu kuliko wanyama wote waishio juu ya uso wa dunia, tunaposema ni mnyama mrefu inatakiwa umuelewe katika sifa yake hiyo, urefu wake ni zaidi ya futi 15,
urefu wake huo lakini pia mkia wake ni mfupi hauwezi zidi cm 90 yaani rula tatu, si mkia tuu hata miguu yake ya nyuma ni mifupi kuliko ya mbele, lakini kwa ujumla miguu yake na shingo ndio humfanya awe mrefu zaidi.
Hubeba mimba ndani ya miezi kumi na tano, na huzaa mtoto mmoja baada ya kipindi hicho, twiga hujifungua akiwa amesimama tuu, na huzaa mtoto mrefu sana, mtoto ambaye huwa na kilo zaidi ya 50, ndani ya saa kadhaa mtoto wa twiga huanza kufanya mazoezi ya kukimbia, katika kipindi hiki mama huwa mlinzi mzuri wa mwanaye.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.