Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Inasadikika nyama ya kiumbe huyu ni tamu pasina mfano, laiti kama uhifadhi usingekuwepo basi wanyama hawa wangekuwa walishakwisha, katika kuthibitisha hilo si binadamu tuu bali karibia wanyama wote walao nyama humuwinda twiga kwa udi na uvumba, na kwakuwa mkubwa hakamatiki basi wanyama hao huwawinda watoto wa twiga tuu.
 
Kiumbe huyu ana ulimi mrefu sana, humsaidia kula majani ambayo yamemea katika miti yenye miba, ni mnyama anayehusudu sana misosi anaweza kula hadi kilo 50 na ushee, pia ni wanyama ambao hawaamini katika kuishi katika mipaka,
 
445212244_219827.jpg
 
kwa lugha nyepesi ni mnyama anayeishi kwa kuhama hama na hii ni kutokana na kutafuta chakula kwani hutumia chakula kingi sana, hasumbuliwi sana na kiu, hivyo maji sio ishu sana ikiwa kama atapata majani yenye unyevu nyevu.
 
Ngozi yake hutumika kutengenezea nakshi ya mavazi ya wakubwa huko duniani, lakini pia ngozi hiyo hiyo ni tiba kwa wataalamu wetu wa mila huku Afrika.
 
Muone mwembamba vile vile lakini ni mzito sana, ana kilo zaidi ya 500 na kadri anavozidi kukua hufika hadi 800 kg, umri wake wa kuishi ni miaka 25 tuu, ambapo kama atafikisha umri huo basi atakufa kwa uzee au kukamatwa kizembe na chui au mamba.
 
Ukiwaona unaweza kuwatofautisha kwa kuwatizama kichwani, Dume huwa na pembe fupi sana ambazo unaweza usizione kama hautakuwa makini kwani huwa na urefu wa nchi tano tuu, na jike hukosa kabisa au huchomoza kidogo sana kutokana na umri.
 
Twiga ni mnyama mrembo mbali na kuwa na haiba ya kuvutia kwa urefu wake, lakini pia ana ngozi yenye rangi nzuri, macho yake ni makubwa na anajua kuyatumia vyema kutizama jambo ambalo humuongezea sifa
 
na dume huwatambua kwa kutizama mkojo wake tuu, mnyama huyu ana uwezo mzuri wa kukimbia ila ni miongoni mwa wanyama ambao wanajichochea yaani kwa kadri anavyokimbia ndivyo spidi yake inaongezeka wenzie wenye sifa hiyo ni pamoja na mbuni, tembo nk.
 
SIFA ZAKE ZA KIPEKEE ********* 1. Ni mnyama mrefu kuliko wote waishio ardhini. 2. Ni mpenda amani sana. 3. Ni mnyama ambaye wanyama wenzie wanaokula majani hujisikia amani sana kukaa naye kwakuwa huona hatari tangu ikiwa mbali, sasa usishangae akina pimbi swala wakijaa chini yake. 4. Akikupiga teke lake ukipona ujue unaweza dondoka ghorofani na ukapona, na hii ndiyo sababu wanyama kama simba na jamii yao hawamsogeleagi kijinga.
 
5. Anatumia miguu ya mbele kama silaha yake wakati wa mapigano, nyuma hutumia inapibidi kama anapambana na mnyama zaidi ya mmoja ila ni nadra sana. 6. Anahusudu sana misosi huyu jamaa hii sekta yupo vizuri sana. 7. Ni mnyama mtalii anapenda sana kushangaa ulimwengu ulivyo na ndio maana hutumia muda wake mwingi katika kutembea. 8. Wakati wanyama wengine wakitumia muda mwingi kulala, pengine twinga ndio kiumbe pekee ambaye hulala muda mfupi kuliko viumbe wengine wote yeye hutumia masaa mawili tuu na kama ana mtoto ndio yatakuwa pungufu ya hapo katika masaa 24 yaani siku.
 
10. Shingo yake ndio sehemu inayomsisimua kimahaba, hivyo siku na mkwe wako mkawa mnawatizama ukiona wameanza kugusana gusana shingo, kuzifunga pamoja mwambie dereva haraka akupeleke upande wa tembo maana ndio majilani zake wakubwa. 11. Twiga jike ni muaminifu sana kwa dume lake, na ili lisimuache mda wake wa ziada hutumia kulishawishi dume limpande, jike hutafuta dume jingine endapo dume wake atakamatwa na mamba au chui au kufa kwa ugonjwa na kama atakosa anaweza kufa kwa upweke, hivyo watu wa hifadhi hufanya juu chini kumuunganishia na madume ambayo nayo yana upweke, inaposhindikana baadhi ya nchi huwatoa polini na kuwaweka chini ya uangalizi maalumu.
 
Back
Top Bottom