Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jiwe la pembe za kulungu
Jiwe hili huwa kubwa sana na huchukua nafasi kubwa kwenye figo.Hufanana na pembe za kulungu. Halisababishi maumivu na mara nyingi halitambuliki na hivyo mwishowe huharibu figo.
 
Nini husababisha mawe ya figo?
Kila mtu anaweza kupata mawe kwenye figo.Hata hivyo, kuna mambo kadha yanayochangia hali hii:

Kutokunywa maji ya kutosha.
Historia ya familia kupata mawe ya figo.
Kula vyakula vyenye nyama, sodiam, oxalate na maziwa mengi na kukosa mboga na matunda.
 
Nini husababisha mawe ya figo?
Kila mtu anaweza kupata mawe kwenye figo.Hata hivyo, kuna mambo kadha yanayochangia hali hii:

Kutokunywa maji ya kutosha.
Historia ya familia kupata mawe ya figo.
Kula vyakula vyenye nyama, sodiam, oxalate na maziwa mengi na kukosa mboga na matunda.
 
Asili mia 75% ya mawe kwenye figo na asili mia 95% ya mawe kwenye kibofu cha mkojo huwapata wanaume kati ya umri wa miaka ishirini na sabini na sanasana walio na uzito mkubwa.
Watu wanaoishi sehemu kavu/kame zenye joto jingi.
Watu ambao hawajiwezi na muda mwingi wamelala (bed ridden/ immobile).
 
Maambukizi ya njia ya mkojo ya mara kwa mara,au kuzibika kwa njia ya mkojo.
Magonjwa kama ya tezi dundundio(thyroid), jongo, na mengineyo yanayotokana na kasoro katika uvunjajivunjaji wa kemikali mwilini.
Matumizi ya dawa fulani fulani kama vile za kukojoa au za kuzuia asidi(diuretics na antiacids).
 
Dalili za mawe katika mfumo wa mkojo ni nini?
Dalili zinazojitokeza hutofautiana kulingana na ukubwa wa jiwe,umbo na mahali lilipo.Dalili zenyewe huwa ni kama zifuatavyo:

Maumivu ya tumbo.
Kukosa dalili zozote na hali hii Hujulikana mtu anapopimwa kwa sababu nyingine. Haya mawe huitwa ‘mawe kimya’.
 
Kukojoa na kuhisi kutaka kukojoa kila mara.
Kichefuchefu na kutapika.
Kukojoa damu(haematuria).
Uchungu au kuwashwa unapokojoa.
Kama jiwe likikwama kwenye njia ya mkojo,mkojo hukatika ghafla wakati wa kukojoa.
Kukojoa jiwe.
 
Wakati mwingine jiwe husababisha matatizo kama maambukizi yanayo jirudia rudia kwenye njia ya mkojo, kufunga njia ya mkojo na hivyo kuleta madhara ya muda au ya kudumu kwenye figo ambayo yakakosa kurekebishika.
 
Maumivu ya tumbo yanayosababishwa na jiwe katika mfumo wa mkojo
Ukali ya maumivu huwa tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine ikitegemea aina,ukubwa na mahali jiwe lilipo.Kumbuka maumivu hayalingani na ukubwa wa jiwe . Jiwe dogo lisilo laini husababisha maumivu makali kuliko jiwe kubwa ambalo ni laini.
 
E7960BD2-14DE-4C38-A5DD-E86693D08DDC.gif
 
Maumivu yanaweza kuwa si makali sana.Maumivu huzidi mtu anapogeuka na yanaweza kukaa kwa dakika au hata saa kadhaa kIsha yakaisha.Huja yakipotea.
Maumivu hutokea upande ulio na jiwe.Maumivu huanzia kwenye kiuno hadi kwenye kinena, yakiambatana na kichefuchefu na kutapika.
 
Jiwe kwenye kibofu pia husababisha maumivu kwa upande wa chini wa tumbo na maumivu wakati wa kukojoa sanasana kwenye uume.
 
Back
Top Bottom