Maradhi haya baadaye huenda katika ini hivyo kumtia matatizo mgonjwa na kwa hakika hali ikifikia hivyo huwa ni hatari.
Saratani ya mapafu huwa ndiyo chanzo kikuu cha mtu kupatwa na saratani ya mifupa ikienea sehemu zote mwilini.
NINI HUSABABISHA KUUGUA MARADHI HAYA
Zipo sababu nyingi za mtu kuugua saratani ya mapafu lakini uvutaji wa sigara, bangi au dawa za kulevya ni moja ya njia ya kusababisha mtu kuugua maradhi haya japokuwa kuna baadhi ya watu huwa wanarithi ugonjwa huu
VIPIMO
Vipimo vya kubaini kama mtu ana saratani ya mapafu au la vipo vingi, daktari anaweza kuamua kutumia kipimo kiitwacho kitaalamu CT au kipimo kingine kiitwacho X – rey ambapo mgonjwa atapigwa picha na chombo hicho sehemu ya kifuani.
Uchunguzi huo utaweza kumfanya daktari kugundua kama saratani hiyo ya mapafu ipo katika pafu moja au mapafu yote na ataweza kujua kama mgonjwa ana seli zisizo ndogo au seli ndogo na atajua kama ugonjwa huo umeenea sana mwilini au la!
TIBA
Tiba ya saratani hii hutegemea uchunguzi ambao utagundua ni kwa kiasi gani mtu ameathirika, daktari anaweza kuamua kufanya upasuaji au kwa kutumia mionzi maalum ya kutibu maradhi haya na akigundua kuwa ugonjwa umeenea sehemu mbalimbali za mwili wa mtu anaweza kutumia njia zote kwa mgonjwa mmoja.

USHAURI
Ni vema kila mtu akawa na kawaida ya kupima afya yake kwani magonjwa mengi yanapogundulika mapema katika mwili tiba yake huwa ni rahisi kwa daktari kuutokomeza ugonjwa na pia huwa nafuu kwa mgonjwa kwa kuwa hata gharama ya tiba huwa ni ndogo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.