UKICHINJA kuku nyumbani cha kwanza ni kuangalia nyongo isiingie kwenye nyama. Kwa upande wa wanyama mfano ng’ombe au mbuzi pia umakini unatakiwa ili isichafue kitoweo.
Nyongo ya ng’ombe licha ya kuzagaa na kutupwa kwenye machinjio mengi ya mifugo ni dawa. Ndiyo inayohusika kutengeneza vitendanisha (reagensts) vya kuchunguza uwapo wa wadudu wanaosababisha magonjwa ya kuhara.
Ndani ya maabara za tiba duniani nyongo, inatengeneza kitendanishi kiitwacho Brillian Green Bile Broth kinachotumiwa kuthibitisha kuwapo au kutokuwapo kwa kimelea cha Escherichia coli kinachoishi ndani ya tumbo la wanyama na wanadamu.
Kwa mujibu wa mtandao wa ://www.cdc.gov (kituo cha kudhibiti maradhi), Escherichia coli (E. coli) ni kimelea kinachosababisha kuhara kuanzia damu hadi kuharisha makamasi.
Ndani ya kundi hili la E choli kuna vimelea vinasababisha maambukizi ya magonjwa ya njia ya mkojo (UTI), homa ya nimonia au vichomi na magonjwa mengine hatari ya tumbo.
Haya ni magonjwa ambayo yanawasumbua Watanzania wengi kwa hiyo kwa kutumia nyongo za ng’ombe wengi wanaofugwa nchini, inawezekana huo ukiwa ni uwekezaji mwingine kwenye sekta ya afya.
Nyongo kukusanywa ili kutumiwa maabara si jambo geni . Enzi za kiwanda cha Tanganyika Packers ilikuwa inakusanywa na kuuza nje haikutupwa kama inavyofanyika sasa kwenye machinjio.
Akitoa maelezo kuhusu nyongo, Sirilo Muganyizi, aliyekuwa mfanyakazi wa zamani wa kiwanda cha Tanganyika Packers kilichokuwa kinachinja na kusindika nyama, anasema ndani ya ng’ombe hutupi kitu.
Mganyizi ambaye alikuwa mfanyakazi wa kiwanda cha TPL kuanzia mwaka 1965 hadi kilipokufa mwishoni mwa miaka ya 80 anasema nyongo ni ajira kwa vijana na ni chanzo cha mapato kwa taifa.
Jijini Dar es Salaam wastani wa ng’ombe 1,000 hichinja kila siku na shehena kubwa ya nyongo hutupwa huko machinjioni kwa sababu hakuna uwekezaji. Serikali iangalie rasilimali hii isipotee
Mkoani Mara, baadhi ya jamii zinatumia kichuri ambao ni mchanganyiko wa kienyeji (kachumbari), unaotengenezwa kwa nyongo, pilipili na kinyesi kilichobaki ndani ya utumbo wa ng’ombe baada ya kuchinjwa.
Walaji wanamini kuwa kachumbari hiyo, huongeza hamu ya kula nyama lakini pia husaidia utumbo kusaga chakula na kupunguza kuvimbiwa , japo sina uhakika na maelezo hayo.
Kichuri husaidia walaji kuendelea kula nyama zaidi na kufurahia kitoweo hicho.
Ukiangalia katika mambo ya matibabu wenyeji wa Mara hawajakosea kula nyongo kwa vile ni malighafi ya dawa za binadamu, lakini kula nyongo bila kuichunguza iwapo ina athari ni hatari zaidi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.