PIZZA CAKE . . MAHITAJI . 480 gram unga wa ngano . sukari kijiko kikubwa cha chakula2 . kijiko kikubwa cha chakula Baking Powder1 kijiko kidogo cha chai Dried Basil1 kijiko kidogo cha chai chumvi1/2 kijiko kidogo cha chai Baking Soda240 gram Cheddar cheese kata cubes 180 gram mtindi halisi 60 gram maziwa ya maji4 ute mweupe wa yai 60 gram siagi iliyoyeyushwa120 gram mchanganyiko wa kitunguu, pilipili hoho, nyanya na bilinganya chop chop60 gram Pizza Sauce120 Mozzarella cheese iliyokwaruzwa JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI Washa moto wa oven nyuzi joto (200 C). Chukua bakuli kubwa safi na kavu kasha changanya unga wa ngano, sukari, baking powder, salt, basil and baking soda Changanya vizuri ichanganyike kasha tupia katika mchanganyiko wako vipande vya cheddar cheese. Chukua bakuli jingne na weka mtindi, ute mweupe wa yai na siagi piga piga mpaka ichanganyike vizuri. Chukua mchanganyiko wa mtindi na mayai kisha mwagia kwenye mchanganyiko wenye unga wa ngano. Hakikisha una changanya vizuri pole pole ichanganyike vizuri. Don't be too rough, hakikisha inachanganyika vizuri na unga wote umelowana kusiwe na unga mkavu au mabonge bonge. Tupia mboga majani na uendelee kuchanganya Sasa mchangayiko wako utakua mzito na safi kabisa Chota mchanganyiko wako na kisha weka kwenye muffin cups. Hakikisha kabla ya kuweka mchanganyiko wako unapaka mafuta katika hizo cups ili pizza yako isishike baada ya kuiva. Chota pizza sauce 1 kijiko kidogo cha chai kisha weka juu ya kila moja wapo Mwisho unachukua ile mozzarella cheese ilyokwaruzwa na unamwagia kwa juu. Choma katika oven kwa dakika 20 Choma mpaka upate rangi ya kahawia au mpaka ukichoma toothpick katikati inatoka safi kabisa. Kisha toa katika oven na iache ipoe kwa dakika 5 kabla hujazitoa kwenye tray uliochomea, Zikishapoa muonekano ndio huo weka juu ya mweza kisha anza kuzitoa moja moja. Unaweza kuigandisha pizza hii kwenye freezer tumia an airtight container na inaweza kukaa kwa mwezi mzima; siku ukitaka kula basi toa kwenye freezer na yeyusha katika joto la chumba au room temperature pole pole