Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

PIZZA CAKE . . MAHITAJI . 480 gram unga wa ngano . sukari kijiko kikubwa cha chakula2 . kijiko kikubwa cha chakula Baking Powder1 kijiko kidogo cha chai Dried Basil1 kijiko kidogo cha chai chumvi1/2 kijiko kidogo cha chai Baking Soda240 gram Cheddar cheese kata cubes 180 gram mtindi halisi 60 gram maziwa ya maji4 ute mweupe wa yai 60 gram siagi iliyoyeyushwa120 gram mchanganyiko wa kitunguu, pilipili hoho, nyanya na bilinganya chop chop60 gram Pizza Sauce120 Mozzarella cheese iliyokwaruzwa JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI Washa moto wa oven nyuzi joto (200 C). Chukua bakuli kubwa safi na kavu kasha changanya unga wa ngano, sukari, baking powder, salt, basil and baking soda Changanya vizuri ichanganyike kasha tupia katika mchanganyiko wako vipande vya cheddar cheese. Chukua bakuli jingne na weka mtindi, ute mweupe wa yai na siagi piga piga mpaka ichanganyike vizuri. Chukua mchanganyiko wa mtindi na mayai kisha mwagia kwenye mchanganyiko wenye unga wa ngano. Hakikisha una changanya vizuri pole pole ichanganyike vizuri. Don't be too rough, hakikisha inachanganyika vizuri na unga wote umelowana kusiwe na unga mkavu au mabonge bonge. Tupia mboga majani na uendelee kuchanganya Sasa mchangayiko wako utakua mzito na safi kabisa Chota mchanganyiko wako na kisha weka kwenye muffin cups. Hakikisha kabla ya kuweka mchanganyiko wako unapaka mafuta katika hizo cups ili pizza yako isishike baada ya kuiva. Chota pizza sauce 1 kijiko kidogo cha chai kisha weka juu ya kila moja wapo Mwisho unachukua ile mozzarella cheese ilyokwaruzwa na unamwagia kwa juu. Choma katika oven kwa dakika 20 Choma mpaka upate rangi ya kahawia au mpaka ukichoma toothpick katikati inatoka safi kabisa. Kisha toa katika oven na iache ipoe kwa dakika 5 kabla hujazitoa kwenye tray uliochomea, Zikishapoa muonekano ndio huo weka juu ya mweza kisha anza kuzitoa moja moja. Unaweza kuigandisha pizza hii kwenye freezer tumia an airtight container na inaweza kukaa kwa mwezi mzima; siku ukitaka kula basi toa kwenye freezer na yeyusha katika joto la chumba au room temperature pole pole
 
JINSI YA KUPIKA KABICHI ILIOCHANGANYWA NA MAYAI . Kabichi ni aina ya mboga za majani ambayo hupikwa kwa mapishi tofauti. Unaweza kupika kabichi yenyewe bila kuchanganya na chochote pia unaweza kupika kwa kuchanganya na nyama, mayai au chochote unachoona kinafaa mboga yako itakuwa nzuri na kuweza kuliwa na ugali, wali na hata kupikia pilau. Leo tutaangalia jinsi ya kupika kabichi iliyochanganywa na mayai, ambapo tunaanza na mahitaji pamoja na hatua za kufuata katika upikaji wa kabichi iliyochanganywa na mayai. -MAHITAJI · Kabichi moja ya ukubwa wa wastani · Mayai manne (4) · Mafuta robo lita · Vitunguu vinne (4) · Karoti kubwa moja · Pilipili manga kiasi · Chumvi kiasi kwa ladha JINSI YA KUPIKA KABICHI HATUA KWA HATUA 1. Chukua kabichi ulikatekate kisha ulioshe. 2. Washa jiko lolote ulilonalo liwe la mkaa, gesi au umeme. 3. Kisha bandika kabichi ulilolikatakata na kuliosha liache liive kidogo kisha ipua. 4. Menya nyanya, katakata vitunguu, karoti uviweke tayari kwa mapishi. 5. Bandika sufuria jikoni na utie mafuta ya kupikia, yakipata moto tia vitunguu ukaange mpaka vibadilike rangi kisha tia nyanya ukaange. 6. Nyanya zikishaiva tia karoti kaanga kidogo. 7. Baada ya hapo tia pilpili manga pamoja na kabichi ulilolichemsha. 8. Vunja mayai uliyoandaa na kisha changanya na kabichi ililoungwa tayari na ukoroge hadi mboga yako ikauke. Mpaka kufikia hapo mboga yetu ya kabichi iliyochanganywa na mayai itakuwa imeiva na tayari kwa kuliwa kwa chakula ukipendacho iwe ugali, wali hata pilau.
 
JINSI YA KUANDAA KACHORI AU KATLESS KACHORI . . MAHITAJI 300 gram nyama ya kusaga 1 kilo ya viazi ulaya (5-6) 1 kijiko cha chakula Mafuta ya kupikia ½ kijiko kidogo cha chai Cumin seeds (Jeera) 1 ½ kijiko kidogo cha chai Coriander powder (Dhaniya) 2 pili pili mbuzi au ndefu za kijani 1 ½ Tangawizi mbichi ¼ Kijiko cha chai Garam Masala 4 kijiko kikubwa cha chakula maji ya limao au ndimu ½ chumvi 10 gram kitunguu swaumu 5 mayai ya kuku Mafuta kwajili ya kukaangia JINSI YA KUTENGENEZA Chemsha viazi kwenye pressure cooker au sufuria vikiwa na maganda yake. Chemsha nyama ya kusaga na maji 50 gram, kitunguu swaumu 10 gram na vijiko 4 vya mai ya limao mpka iive kisha weka pembeni. Kisha menya viazi ulivyochemsha kisha kata katika vipande vidogo. Pasha mafuta ya kupikia kijiko kimoja kwenye kikaango. Kisha weka mbegu za cumin kwenye kikaango. Mbegu za cumin zikishapasuka, ongeza coriander powder, pili pili mbuzi, Tangawizi, Kisha weka chumvi na viazi. Kaanga kwa dakika 2-3 itakua imeiva vizuri. Kisha ponda mchanganyiko wako mpaka uwe laini kabisa Kisha chukua mchanganyiko huo laini wa viazi na tengeneza maumbo madogo ya mviringo ukubwa kama limao kisha bonyeza kwa kutumia kidole kati kati ya umbo hilo utapata nafasi ya kuweka kijiko kimoja cha chai nyama ya kusaga iliyoiva kisha funika kwa kutumia viazi na jitaidi kuviringisha tena kwa kutumia mikono yako miwili ili upate umbo zuri. Baada ya kumaliza kuandaa maumbo safi kabisa ya duara na yenye nyama ya kusaga kwa ndani, piga mayai pembeni kwenye bakuli na chovya umbo moja moja na weka kwenye kikaango chenye mafuta ya moto kaanga ukishapata rangi tu ya kahawia toa maana viazi na nyama vimeshaiva unachotafuta ni kau kau na rangi safi ya kahawia pande zote. MPATIE MLAJI KACHORI HII IKIWA YAMOTO PIA UNAWEZA USIWEKE PILI PILI NA TANGAWIZI HASA KWA WALE WANOSUMBULIWA NA VIDONDA VYA TUMBO AU MATATZIZO YA GESI TUMBONI NA BADO KACHORI YAKO IKAWA SAFI SANA. UNAWEZA KULA NA TOMATO SAUCE, MAYONAISE, CHACHANDU AU ACHALI.
 
Simple mayonise salad . . Carot 2 Hoho 2 Matango 2 Pilipili manga kidg Ndimu kipande Mayonise . . Safisha vitu vyako vizur kisha vikate kwa urefu kama chipsi ila ziwe nyembamba na vyote jitahidi viwe urefu sawa itapendeza zaid weka katika bakuli tia chumvi kdg na pilipili manga pamoja na ndimu kisha weka mayonise utakisia kwa wewe unavopenda ikolee kama unataka kidg au ienee haswa ila kila ikikolea ndio utamu inazidi ikiwa tyr andaa kwa kula ni tamu sana. Ikiwa ni mpz wa vitunguu maji unaweza kueka lakini ukiweka tu uwe tyr kwa kuila usipende kuiweka vinalinika vinakua havipendezi.
 
JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA KACHORI. Mahitaji Viazi mbatata (potato 4 vya wastani)Nyama ya kusaga (mince beef 1 kikombe cha chai)Kitunguu (onion 1 cha wastani)Carrot 1Hoho (green pepper 1/2)Kitunguu swaum (garlic)Tangawizi (ginger )Binzari nyembamba (ground cumin 1/2 kijiko cha chai)Binzari manjano (turmeric 1/2 kijiko cha chai)Curry powder 1/2 kijiko cha chaiLimao (lemon 1/2)Pilipili ya unga (chilli powder 1/2 kijiko cha chai)Giligilani (coriander kiasi)Chumvi (salt)Mafuta (vegetable oil)Unga wa ngano kiasi Matayarisho Katakata vitunguu na hoho katika vipande vidogo vidogo na kisha kwangua carrot na uweke pembeni. Chemsha viazi na chumvi kidogo vikiiva viponde na uviweke pembeni, Baada ya hapo tia nyama limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi ichemshe mpaka iive na uhakikishe maji yote yamekauka. Kisha Tia binzari zote, pilipili, curry powder, giligilani, vitunguu, hoho na carrot. Pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 3 na kisha ipua. Baada ya hapo changanya na viazi kisha tengeneza maduara ya kiasi na uyaweke pembeni. Chukua unga wa ngano kiasi na uchanganye na maji kupata uji usiokuwa mzito au mwepesi sana. baada ya hapo chovya madonge katika huo uji na uyachome katika mafuta. Hakikisha zinaiva na kuwa rangi ya brown na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza ukazisevu na chatney yoyote unayopendelea.
 
JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA MCHUZI WA NYAMA YA KUKU . Vipimo Kuku 1 au pound 4 Vitunguu maji 5 Nyanya/tungule 3 Nyanya kopo (tomatoe paste) 4 vijiko vya supu Tangawizi mbichi ilosagwa 1 kijiko cha supu Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa 1 kijiko cha supu Pilipili mbichi ilosagwa 1 kijiko cha chai Mafuta ½ kikombe Bizari ya mchuzi 1 kijiko cha chai Bizari ya Methi/uwatu ½ kijiko cha chai Chumvi kiasi Ndimu 1 moja kamua Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Mkate kuku vipande vya kiasi, msafishe na mwoshe vizuri weka kando. Katakakata vitunguu, nyanya/tungule (chopped) weka kando. Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga vitunguu hadi viwe vyekundu kukaribia rangi ya brauni ilokoza. Tia tangawizi ilosagwa pamoja na kitunguu thomu, tia bizari zote, kaanga kidogo tu. Tia vipande vya kuku, kaanga ukigeuza huku na kule kwa muda wa dakika 5 takriban. Tia nyanya/tungule na nyanya kopo kaanga kidogo tena, kisha tia maji ya kutosha kuku aive. Acha kwenye moto itokote/ichemke. Tia pilipili mbichi ilosagwa pamoja na ndimu na chumvi. Mwishowe karibu na kuku kuiva Epua ukiwa tayari kuliwa na wali au mkate upendao. Kidokezo: Ni vyema kumsafisha kuku kwa haldi/tumeric/bizari ya manjano au siki ili kukata harufu ya kidusi cha kuku
 
JINSI YA KUPIKA VISHETI KWA URAHSI. Vipimo 1.Unga 2 Vikombe 2.Samli au shortening ya mboga 2 Vijiko vya supu 3.Maziwa ¾ Kikombe 4.Iliki Kiasi 5.Mafuta ya kukarangia Kiasi 6.Shira 7.Sukari 1 Kikombe 8.Maji ¾ Kikombe 9.Vanila ½ Kijiko cha chai 10.Zafarani (ukipenda) Kiasi Namna ya kutayarisha na kupika Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine. 1. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo. 2. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi. 3. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha. 4. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. 5. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote. 6. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.
 
JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA SUPU YA MABOGA Mahitaji Boga moja Kitunguu maji kimoja Kitunguu saumu kilichosagwa vijiko vya chai 2 Maziwa Siagi vijiko 3 Matayarisho 1. Kata kata boga vizuri na kisha toa mbegu zote na ganda la nnje. 2. Weka sufuria jikoni na siagi ikishayeyuka kaanga vitunguu maji, viianza kulainika weka vitunguu saumu na endelea kukoroga hadi viive. 3. Weka vipande vya boga na koroga vichanganyike na vitunguu kisha weka maziwa, chumvi kiasi na funikia uache vichemke katika moto wa wastani. 4. Ukiona inakauka kabla ya kuiva na kulainika ongeza maziwa ila angalia isiwe nzito sana au nyepesi sana. Ikishaiva epua na unaweza iponda ponda kwa kutumia kifaa cha kupondea viazi au ‘food processor’. 5. Supu tayari kwa kula kama mlo wa utangulizi.
 
MAPISHI YA CHAPATI ZA NYAMA . Vipimo Unga 1 ½ vikombe vya chai Mafuta ¼ kikombe cha chai Chumvi ½ kijiko cha chai Maji 1 kikombe cha chai Mafuta ½ kikombe cha chai Mayai 6 mayai Manda nyembamba za mraba (Spring roll pastries sheet) 6 Nyama ya kusaga ½ kilo Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi 1 kijiko cha supu Kotmiri iliyokatwakatwa ½ kikombe Chumvi kiasi Pilipili manga ½ kijiko cha chai Pilipili mbichi kiasi (ukipenda) Bizari ya pilau ya unga ½ kijiko cha chai. Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Changanya unga na mafuta ¼ kikombe maji na chumvi pamoja kanda mpaka ulainike Kata madonge sita, mimina mafuta ½ kikombe kwenye chombo kipana kisha yaroweke madonge kwa muda wa ½ saa hadi saa 1. Changanya nyama na vitu vyote na ichemshe mpaka iwe kavu kama nyama ya sambusa , wacha ipoe. Sukuma donge ulitandaze liwe jepesi, kisha weka juu yake hiyo manda nyembamba ya mraba . Kwenye bakuli ndogo piga yai moja na vijiko 2 vya hiyo nyama kavu kisha mimina juu ya hiyo manda ya mraba kisha ifunike kama inavyoonyeshwa kwenye picha. Choma kama unavyochoma chapati ila wakati unageuza kutia mafuta toboa toboa na uma ili yai lipate kuiva vizuri ndani kwa moto wa kiasi. Weka kwenye sahani tayari kuliwa.
 
SIMPLE DESSERT. Mahitaji Matunda mchanganyiko (mix fruit) kama vile Ndizi Zabibu Pears (liliova laini) Nanasi Strawberry Embe Yogurt kiasi Asali Cinnamon powder kidogo sana (1/4 ya kijiko cha chai) Matayarisho Safisha matunda yote kisha yakaushe maji baada ya hapo yakate katika vipande vidogo vigogo kisha yatie kwenye bakuli safi.Baada ya hapo tia cinnamon na yogurt vichanganye vizuri kisha sawazisha. Malizia kwa kumwagia asali juu yake (kama uonavyo kwenye picha) Unaiweza kuila baada ya hapo au ukaiweka frijini ipate baridi na ikaliwa baadaye. Dessert hii ni rahisi kutengeneza pia ni nzuri kwa afya ya mlaji kwa sababu haina sukari pia ina matunda. Kwa hiyo ni vizuri zaidi wakati mwingine una avoid ice cream kwa dessert na kutumia hii.
 
MAPISHI YA BAJIA ZA KUNDE . . VIPIMO . Kunde za kupaaza 1 ½ Vikombe Vitungu vya kijani iliyokatwa katwa ½ Kikombe Baking soda ¼ Kijiko cha chai *Bizari mchanganyiko 1 Kijiko cha chai Maziwa 2 Vijiko vya supu Chumvi 1 ¼ Vijiko vya chai Unga wa ngano 2 Vijiko vya supu Mafuta ya kukaangia * Unaweza kutumia bizari ya pilau (cummin) ukipenda NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA Osha na kuroweka kunde kwenye bakuli la maji ya baridi usiku mpaka asubuhi. Saga kwenye mashine (food processor) kisha mimina kwenye bakuli. Ongeza vitungu, baking soda, masala, maziwa, na chumvi. Koroga vizuri halafu tia unga kisha uchanganye pamoja. Fanya vidonge kama nchi moja kisha ukipenda bana katikati ya mikono na kidole katikati ya bajia. Kaanga kwenye mafuta ya moto mpaka ziive. Andaa bajia kwenye sahani nA tayali Kwa kuliwa
 
MCHUZI WA SAMAKI WA EMBE NA NAZI Mahitaji:- King fish alooshwa na kukatwa vipande vikubwa kiasi 350 Embe lilokatwa vipande vyembamba1 Rojo la ukwaju (Tamarind paste) kjk 1 chai Kitunguu kilichokatwa 1 Tangawizi ilokatwa 1 Kitunguu saumu kilichokatwa 1 Pilipili za kijani 5-6 ukipenda Nyanya zilizokatwa 2 Pilipili nyekundu ya unga kjk 1 1/2 chai Manjano 1/2 kjk chai Tui la nazi zito kikombe 1 Maji kikombe 1 Uwatu 1/2 kjk chai Majani ya cury jani 2 Kotmir(giligilani ilokatwa 1/2 kjk chai Mafuta ya nazi vjk 2-3 chakula Chumvi kiasi JINSI YA KUPIKA 1.Tia sufuria ya mafuta au frying pan kubwa jikoni, ktk medium heat. 2. Tia uwatu kisha acha uchemke 3. Tia majani ya curry yalokatwa,kitunguu,tangwizi,saumu na pilipili za kijani kisha kaanga vzr had vitunguu viwe brown. 4. Tia nyanya na kaanga hadi ziwe laini kisha ponda au saga kupata rojo. 5. Tia pilipili ya unga,manjano,ukwaju kisha kaanga kidogo, tia maji kisha cha ichemkie. 6. Tia vipande vya samaki kisha zungusha sufuria kuchanganya, tia chumvi kisha acha ichemkie kdg. 7.Tia vipande vya embe na pika kwa dk kadhaa. 8. Tia tui na kotmir punguza moto uwe mdogo kisha acha itokote kwa dk kadhaa. Mchuzi tayari kula na wali.
 
MCHUZI WA SAMAKI WA EMBE NA NAZI Mahitaji:- King fish alooshwa na kukatwa vipande vikubwa kiasi 350 Embe lilokatwa vipande vyembamba1 Rojo la ukwaju (Tamarind paste) kjk 1 chai Kitunguu kilichokatwa 1 Tangawizi ilokatwa 1 Kitunguu saumu kilichokatwa 1 Pilipili za kijani 5-6 ukipenda Nyanya zilizokatwa 2 Pilipili nyekundu ya unga kjk 1 1/2 chai Manjano 1/2 kjk chai Tui la nazi zito kikombe 1 Maji kikombe 1 Uwatu 1/2 kjk chai Majani ya cury jani 2 Kotmir(giligilani ilokatwa 1/2 kjk chai Mafuta ya nazi vjk 2-3 chakula Chumvi kiasi JINSI YA KUPIKA 1.Tia sufuria ya mafuta au frying pan kubwa jikoni, ktk medium heat. 2. Tia uwatu kisha acha uchemke 3. Tia majani ya curry yalokatwa,kitunguu,tangwizi,saumu na pilipili za kijani kisha kaanga vzr had vitunguu viwe brown. 4. Tia nyanya na kaanga hadi ziwe laini kisha ponda au saga kupata rojo. 5. Tia pilipili ya unga,manjano,ukwaju kisha kaanga kidogo, tia maji kisha cha ichemkie. 6. Tia vipande vya samaki kisha zungusha sufuria kuchanganya, tia chumvi kisha acha ichemkie kdg. 7.Tia vipande vya embe na pika kwa dk kadhaa. 8. Tia tui na kotmir punguza moto uwe mdogo kisha acha itokote kwa dk kadhaa. Mchuzi tayari kula na wali.
 
JUISI YA UKWAJU .. . Ukwaju kiasi Sukari robo Hiliki kijiko 1 Maji kiasi Tangawizi mbichi 1/2 kijiko iliosagwa JINSI YA KUANDAA 1.Chemsha ukwaju, ukipoa ,tia tangawizi ufikiche pamoja na ukwaju kisha ukamue rojo lote ,uuchuje 2.Saga iliki ziwe unga kisha tia katika juisi pamoja na sukari kisha koroga mpaka sukari ikolee vizuri 3.Weka katika fridge ikipata baridi tayari kwa kunywa na vitafunio au chakula chochote upendacho.ENJOY!!! NB: Waweza tia arki ya rose au vanilla ya maji kuongeza harufu au kama hupendi hiliki.Juisi ya ukwaju husafisha mkojo,pia nzuri kwa wanaopata choo kigumu.
 
JINSI YA KUPIKA JAM YA NANASI . . MAHITAJI ♦Nanasi kata vipandevipande ♦sukari nyeupe au yakawaida vikombe 2 ♦ndimu vijiko 4 ♦maji kikombe 1 JINSI YA KUPIKA 1.Chemsha nanasi hadi likiwa laini lipondeponde 2.Tia sukari ktk sufuria na maji ukoroge mpaka iyeyuke 3.Iweke jikoni ichemke mpaka uone inanatanata ktk vidole tahadhari isiungue 4.Tia nanasi lako na maji ya ndimu changanya ,iwache ichemke kwa moto mdogo mdogo mpaka iwe nzito kama jam zengine kisha epua ,tayari kwa matumizi waweza kula na mkate,banzi nk.ENJOY!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…