Kuna muuza duka mmoja aliwahi kuniambia, “Wanaokuja kununua dawa bila kuwa na cheti kinachoonyesha vipimo kutoka kwa daktari huwa nawashauri waende hospitali kwanza wakapime, ila kuna tatizo kubwa, mtu anakwambia we nipe tu dawa mimi ndiyo ninayeumwa na najua ninachoumwa wewe nipe dawa ninazotaka.”