Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kutokana na hilo, Mata akaamua kuondoka Chelsea na kwenda Manchester United ambako bado yupo hadi sasa. Wanasema binadamu hukutaka na sasa, Mata na Mourinho wamekutana tena Old Trafford na sasa wawili hao wanaonekana kutokuwa na tofauti licha ya kwamba bado Mhispaniola huyo amekuwa hamalizi dakika zote tisini anapochezeshwa huko Man United.
 
Rafael da Silva v Louis van Gaal (Man United)

Mashabiki wa Ligi Kuu England hawakumwelewa kabisa kwanini kocha Mdachi, Louis Van Gaal aliamua kumpiga bei beki wa kulia wa timu hiyo, pacha wa Kibrazili, Rafael da Silva. Van Gaal aliamua kumuuza Mbrazili huyo kwenye Olympique Lyon ya Ufaransa huku nyuma akiacha pengo kubwa kwenye kikosi cha Manchester United.
 
Asikwambie mtu, Rafael alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Man United kutokana na soka lake la kujitolea alilokuwa akicheza kwenye kikosi hicho. Hakuwa akipenda kabisa Man United ipoteze mechi ndio maana uchezaji wake ulikuwa wa kujitolewa kwa zaidi ya asilimia 100 kama alivyokuwa akifanya Ander Herrera anapopewa nafasi ya kucheza. Kocha Sir Alex Ferguson alimsajili Rafael na pacha wake, Fabio wakati wote wakiwa na umri wa miaka 18 na hivyo walikuwa kwenye kikosi hicho na kuufahamu vyema utamaduni wa timu hiyo yenye maskani yake Old Trafford. Rafael alijitengenezea nafasi kwenye kikosi cha kwanza na kuwa panga pangua akiwa chaguo la beki wa kulia na karibu alicheza kila mechi katika msimu wa mwisho wa Ferguson. Lakini, kwa ujio wa Van Gaal tu Old Trafford ulibadili upepo na Rafael akaonekana hafai.
 
Joe Hart v Pep Guardiola (Man City)

Wengi walishangaa sana uamuzi wa kocha mpya wa Manchester City, Pep Guardiola kuamua kumtoa kwa mkopo aliyekuwa kipa namba moja kwenye kikosi hicho, Joe Hart. Hakuna mtu ambaye hakushangazwa na tukio hilo muda mfupi tu baada ya Mhispaniola huyo kutua kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England akitokea kwenye Bundesliga.
 
Kitendo cha Guardiola kutua kwenye kikosi cha Man City huko Etihad, akaamua kumwondoa Joe Hart na kisha kumchukua kipa wa Barcelona, Claudio Bravo. Joe Hart hakuwa na maisha tena Etihad na alitolewa kwa mkopo wa msimu mzima kwenda Torino inayoshiriki ligi ya Serie A huko Italia. Msimu ulipomalizika alirudi Man City, lakini akatolewa tena kwa mkopo mwingine kwenda West Ham United. Kitu kilichowashangaza wengi ni kitendo cha Guardiola kumwondoa Joe Hart na kumleta Bravo, ambaye kiwango chake kimeonekana wazi kabisa kwamba si cha kufurahisha kihivyo. Guardiola akaamua kufanya mabadiliko mengine kwenye nafasi ya makipa akimchukua Ederson kutoka Benfica, walau sasa kipa huyo anafanya vizuri.
 
Kaka v Jose Mourinho (Real Madrid)

Mbrazili, Ricardo Kaka alikuwa staa mkubwa sana huko AC Milan akitamba na timu hiyo kwenye Serie A na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Real Madrid wakapanda bei na kwenda kuinasa huduma yake ili akaongeze nguvu katika kikosi hicho katika awamu ya pili ya Galacticos iliporudishwa na Florentino Perez huko Bernabeu.
 
Kipindi Kaka anakwenda Real Madrid timu hiyo ilikuwa chini ya kocha Manuel Pellegrini na hiyo ilikuwa mwaka ambao Mbrazili huyo alikuwa akicheza kandanda malidadi kabisa la kiwango cha juu lililomfanya ashinde tuzo ya Ballon d’Or. Lakini, mwaka mmoja baadaye, Real Madrid ilibadili kocha na kumchukua Jose Mourinho. Mreno huyo baada ya kutua tu Bernabeu akitokea Inter Milan, kitu cha kwanza alichokifanya ni kwenda kumsajili kiungo wa Ujerumani, Mesut Ozil, akimtoa Wender Bremen kipindi hicho katika majira ya kiangazi ya mwaka 2010.
 
Ujio wa Mourinho na Ozil ukaanza kuwa na athari kwa Kaka na maisha yake yalianza kuwa magumu kwenye kikosi hicho. Akawa hapewi muda wa kutosha wa kucheza, Ozil akipangwa zaidi na hilo lilimfanya Kaka sasa kuwa na maisha magumu Bernabeu na kuamua kuondoka akishindwa kutimiza kabisa ndoto zake za kuwa gwiji katika klabu hiyo.
 
Yaya Toure v Pep Guardiola (Man City)

Kwa karibu miaka mitano, kiungo Muivory Coast, Yaya Toure alikuwa mchezaji muhimu kweli kweli kwenye kikosi cha Manchester City na panga pangua alikuwa hakosekani katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Man City ingeweza kuwaweka benchi mastaa wake wote kwa kipindi hicho, lakini si Yaya Toure.
 
Kwenye dirisha la usajili wa majira ya kiangazi la mwaka 2016 kila kitu kilibadilika, mambo yakaanza kwenda tofauti kabisa kwa upande wake baada ya ujio wa kocha Pep Guardiola katika kikosi cha Man City. Guardiola akaanza kumpiga benchi Yaya Toure jambo lililomfanya kiungo huyo kuchukia sana na kuibuka kwa malumbano makubwa yaliyokuja kumhusisha pia wakala wake na hivyo kumfanya Guardiola kupiga mkwara anataka aombwe radhi la sivyo, Yaya Toure asingecheza mechi nyingi tena. Baada ya muda kidogo, Yaya Toure alipewa nafasi ya kucheza kabla ya sasa kurudi tena benchi na kumfanya asahaulike kabisa kama bado ni mchezaji wa timu hiyo na mwaka jana tu hapo alisaini mkataba mpya.
 
Robin Van Persie v David Moyes (Man United)

Sir Alex Ferguson alimsajili straika Robin Van Persie kutoka Arsenal mwaka 2013 na Mdachi huyo baada ya kutua Old Trafford tu alifunga mabao 26 katika mechi 38 alizocheza kwenye Ligi Kuu England na kuisaidia Manchester United kubeba taji lake la 20 la ligi, ambalo ni la mwisho pia kubeba, tangu wakati huo hawajabeba tena.
 
Back
Top Bottom