Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji818]
Screenshot_2018-03-20-18-20-40-1.jpg
 
YAFAHAMUMAGONJWA HATARI YA NYANYA NA DAWA ZAKE
Pamoja na umuhimu wake, magonjwa ya nyanya yamekuwa ni kikwazo kikubwa sana katika uzalishaji na ubora wa matunda ya nyanya. Sasa ili mkulima aweze kupata faida na kuongeza pato lake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa ya nyanya tangu mwanzo zinapoonekana dalili.
 
Utangulizi
Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote (masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa na mazao mengine. Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze kupata faida na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu wa zao hili. Katika makala hii tutaangalia namna ya kudhibiti baadhi ya magonjwa muhimu ya zao la Nyanya.
 
1. Ugonjwa wa Ukungu
(i) Bakajani tangulia au ukungu mapema: Early blight (Alternaria solani)
Dalili
Dalili za ukungu mapema hutokea kwenye matunda, shina, na majani ya nyanya. Majani huonesha madoa ya kahawia iliyokoza na yenye mfumo wa duara zenye kati moja. Madoa kwanza hujitokeza kwenye majani yaliyokomaa na kuendelea juu ya mmea. Majani yenye madoa huweza kufa kabla ya wakati wake na kusababisha kupukutika mapema kwa majani, matunda huungua kwa jua na kuwa na rangi isiyopendeza.
 
Madoa ya kwenye matunda hujitokeza kwa juu kwenye ncha ya shina. Kwa kawaida madoa huwa na rangi ya kahawia iliyokoza mpaka nyeusi, yaliyozama ndani, magumu na yenye duara za kipekee zenye mfumo wa kati moja. Kuoza kwa chini ya shina huweza kutokea kwenye miche michanga. Hali hii hujionyesha kwa kuzunguka shina sehemu ya chini. Miche iliyoathirika hudumaa na huweza kunyauka na kufa. Miche mikubwa iliyoathirika huwa na makovu ambayo kawaida huwa upande mmoja tu wa shina na hurefuka na kudidimia kwenye mashina na vikonyo.
 
Dalili za ugonjwa wa ukungu mapema mara nyingi hudhaniwa kuwa ni ukungu chelewa, lakini kwenye ukungu chelewa makovu yamefifia, madogo na hayana alama za duara zilizonyanyuka.
 
Njia za kudhibiti
Ukungu mapema unaweza kubainika shambani kwa kutafuta madoa ya kahawia iliyokoza ya kiasi cha 1.2 sm kwa upana. Ni vigumu sana kuzuia ukungu mapema ukishaanza shambani. Njia muhimu ya kudhibiti ukungu mapema ni kuzuia kuingia kwake na kusambaa.
 
Mbinu bora za kilimo
•Zungusha mazao ya nyanya na nafaka ndogo ndogo, mahindi au jamii za kunde
•Panda aina zenye kustahimili ‘early blight’. (Km. Floradade, Hytec 36, Julius F1 na Zest F1)
•Tumia mbegu safi
•Limia na kufukia mabaki ya mazao baada ya mavuno na choma moto mazao yaliyoathirika na takataka zote za mazao
•Epuka kumwagilia kwa juu
 
Ongezea mbolea ya samadi
•Tumia matandazo kuzuia kurukia kwa maji
•Hakikisha kupanda kwa nafasi sahihi na kufunga vijiti
•Toa majani ya chini yaliyoathirika ili kuboresha mzunguko wa hewa
•Epuka kutumia ardhi kwa angalau miaka 2 baada ya uzalishaji wa nyanya
 
Ongezea mbolea ya samadi
•Tumia matandazo kuzuia kurukia kwa maji
•Hakikisha kupanda kwa nafasi sahihi na kufunga vijiti
•Toa majani ya chini yaliyoathirika ili kuboresha mzunguko wa hewa
•Epuka kutumia ardhi kwa angalau miaka 2 baada ya uzalishaji wa nyanya
 
Dawa (chemical control)
‘Early blight’ inaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa za ukungu Boscalid ( Endura Captan, Captan 4F, Captan 50), dawa za ukungu zenye shaba (Champ Dry Prill, Champ Formula 2, Copper-Count-N, Kocide 101, Kocide DF, Kocide 4.5LF, Kocide 3000, Nordox Tri Basic), Chlorothalonil na Chlorothalonil Mixtures (Bravo 720/Echo, Bravo Ultrex/Echo 90DF, Bravo Weather Stik, Echo Zn, Ridomil Gold/Bravo), EBDC, Copper FBDC na EBDC/Zaxamide (Cuaprofix Disperss M2, Dithane/Gavel, Maneb 75, Manex, Mankocide, Manzate F1, Penncozeb 80W, Penncozeb 75DF), Famoxadone+Cymoxanil (Tanos, Fenamidone, Reason 500SC, Penthiopyrad, Fontelis, Pyrimethanil, Scala), Strobilurin na Strobilurin Mixtures (Cabrio, Flint, Quadris)
 
Kibaiolojia (Biological control)
Kuna mazao mengi yatokanayo na mimea ambayo husemekana kuwa na sifa za sumu kwa aina nyingi za ukungu. Haya ni mazao asilia ambayo hupoteza nguvu zake haraka juu ya majani na kwenye udongo. Juu ya hivyo, taarifa kidogo sana zinajulikana kuhusu viwango vyao vya matumizi, athari zao juu ya viumbe marafiki, na binadamu.
 
(ii) Bakajani Chelewa au Ukungu chelewa: Late blight (Phytophthora infestans)
Dalili
Dalili za ukungu chelewa hujitokeza kwenye matunda, majani, shina na matawi. Kwenye majani madoa ya kijani kibichi/kahawia hujitokeza upande wa juu wa majani, na pembezoni mwa majani huwa kijani kibichi na huwa kama iliyotota, kwa kawaida madoa hutanuka ghafla hadi majani yote yanapokufa. Nyakati za hewa ya unyevu, ukungu mweupe/kijivujivu hujitokeza kwenye kingo za madoa katika sehemu za chini za majani. Wakati wa joto, sehemu zilizoathirika huonesha kukauka. Madoa ya kahawia na yaliyorefuka hujitokeza kwenye mashina.
 
Kwenye matunda, madoa ya kijivujivu/kijani yaliyotota hujitokeza kwenye nusu ya tunda upande wa juu. Madoa haya baadae husambaa na kugeuka kahawia, yaliyokunjamana na magumu. Wakati wa hali ya unyevu ukungu mweupe hujitokeza kwenye sehemu za matunda yaliyoathirika. Dalili za ukungu chelewa mara nyingi hudhaniwa ni ukungu mapema (Alternaria solani), lakini dalili za ukungu mapema mara nyingi huwa za duara zaidi, kubwa, na zilizokoza na za duara zenye kati moja. Ukungu chelewa hauna duara hizi.
 
Njia za kudhibiti
Nyanya zilizoambukizwa huweza kushambuliwa kwa haraka na kuteketezwa na ukungu chelewa. Kuzuia ugonjwa huu ni shida sana ukishajiimarisha shambani. Njia muhimu sana ya kuzuia ukungu chelewa ni kuhakikisha haijajiimarisha na kusambaa. Hii inaweza kufanyika kwa kutumia mbinu zifuatazo:
 
Back
Top Bottom