Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager imetangaza rasmi promosheni ya Vuta Pumzi Na Safari Ndogo ambapo watumiaji wa bia ya safari watajishindia kinywaji hicho kwenye vituo vya daladala.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Masoko wa Kampuni hiyo, Kabula Nshimo, amesema kuwa promosheni hiyo itahusisha watu walio juu ya miaka 18 na itakuwa siku ya Jumatano pekee.
 
Akifafanua, Nshimo alisema mtumiaji wa bia hiyo atakwenda kwenye vituo vya daladala/mabasi vyenye huduma hiyo ambayo kwa kuanzia wameanza na kituo cha Morocco na baadaye itasambaa vituo vingine vya daladala ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Kumbuka mashine hizo zitatoa bia kwa siku ya Jumatano pekee kuanzia saa 10 jioni hadi saa 6 usiku na washindi wote watapelekwa kwenye baa zilizo karibu na kituo husika.
 
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager imetangaza rasmi promosheni ya Vuta Pumzi Na Safari Ndogo ambapo watumiaji wa bia ya safari watajishindia kinywaji hicho kwenye vituo vya daladala.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Masoko wa Kampuni hiyo, Kabula Nshimo, amesema kuwa promosheni hiyo itahusisha watu walio juu ya miaka 18 na itakuwa siku ya Jumatano pekee.

Promosheni inafanywa saa ngapi ???
 
MAMBO ni magumu na hali ya sintofahamu kuhusiana na mustakabali wa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, imeendelea kushika kasi pale Old Trafford.


Wakati hali ikiwa hivyo, taarifa mpya ni kuwa wababe hao wa Old Trafford wamefuta mpango wa kumsajili straika wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann na badala yake wametua kwa winga wa Real Madrid, Gareth Bale.


Kwa muda mrefu sasa, Man United imekuwa ikimuwinda Griezmann, ambaye kuna wakati ilitangazwa wamefikia makubaliano binafsi, lakini kwa sasa mambo yamebadilika na staa huyo wa Kifaransa anatajwa anaweza kutua Barcelona mwishoni mwa msimu huu.
 
MCHUMBA wa muda mrefu wake fowadi wa Real Madrid, Gareth Bale, kichuna Emma Rhys kadokeza kuwa ile harusi yao iliyoratibiwa kufanyika Desemba mwaka jana, itafanyika mwishoni mwa msimu huu wa ligi.


Kupitia posti kadhaa ambazo amekuwa akitupia kwenye mitandao ya kijamii, Emma anaonekana kuashiria kuwa ndoa yao itafanyika Mei 2018 mara tu baada ya Ligi Kuu kufikia kikomo.
Harusi hiyo ilikuuwa ifanyike Desemba ya mwaka jana ila ikaahirishwa kwa sababu kadhaa wa kadhaa.


Sasa Emma ameweka bayana kwamba mwaka huu hautaisha kabla hajaitwa mke wa mtu. Wapenzi hao wamekuwa wapenzi kwa zaidi ya miaka 10 na kufanikiwa kujaliwa mabinti wawili.
 
MWANAUME hakimbii vita unaambiwa. Jose Mourinho amesema hawezi kukimbia majukumu mazito yanayomkabili kwenye kikosi cha Manchester United kutokana na nyakati ngumu zinazoikabili timu hiyo kwa sasa.

Kocha huyo Mreno amekuwa akikosolewa kila kona kwa mbinu zake kwamba ameifanya Man United kuwa timu ya ovyo baada ya kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Sevilla Jumanne katika hatua ya 16 Bora.
 
Mourinho alileta ujanja ujanja tu wa kujitetea kwamba Man United kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya si mara ya kwanza baada ya mabao mawili ya Wissam Ben Yedder kuwasukuma nje kwa kipigo cha 2-1 licha ya kucheza kwenye uwanja wao wa nyumbani, Old Trafford. Katika kuzijibu tuhuma hizo zinazoelekezwa kwake, Mourinho alitumia dakika 12 mbele ya waandishi wa habari kuwaambia kuhusu nyakati ngumu inazopitia Man United kwa sasa na kuwaambia inachojaribu kukifanya Manchester City kwa sasa wao Man United kwao ni zilipendwa, walishafanya miaka kibao iliyopita.
 
Ninataka niwaambie mashabiki kwamba mashabiki watabaki kuwa mashabiki na uhuru wao wa kutoa maoni na kuhamaki. Lakini, kuna kitu ambacho mara kwa mara nimekuwa nikisema kuhusu urithi wa soka,” alisema.

“Kocha alichokirithi kwenye timu hii, hivi ni lini Manchester United ilicheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya mwisho, ilikuwa mwaka 2011. Tangu mwaka huo, mwaka 2012, waliishia hatua ya makundi na timu ilizopangwa nazo wakati ule ni kama sawa tu na za msimu huu, walipangwa na Benfica, Basel and Galati ya Romania. Wakatolewa hatua ya makundi.
 
Miaka saba ya makocha wanne tofauti, haijawahi hata kufuzu kucheza Europe, ilitolewa mara mbili hatua ya makundi na rekodi yao bora ilikuwa robo fainali, hiyo ndiyo timu niliyoirithi. Ukirudi kwenye Ligi Kuu England, mara ya mwisho kushinda ubingwa ilikuwa 2012/13 na misimu minne iliyofuatia, ikamaliza ya saba, nne, tano na sita. Hivyo kwa miaka minne iliyopita, nafasi bora kwenye ligi ilikuwa nafasi ya nne. Huu ndiyo urithi wa soka tulioachiwa.
 
Hiyo ina maana kwa sasa kila kitu kinaanza kutayarishwa upya, lazima kutakuwa na mapito ya hapa na pale. Hizo ni takwimu za kweli kabisa. Nitawaambia mengine; Miaka saba iliyopita, nafasi mbaya zaidi iliyoshika Man City kwenye Ligi Kuu England ni namba nne. Katika miaka hiyo saba ya mwisho Man City imechukua ubingwa mara mbili, unaweza kusema hii ni mara ya tatu, lakini wamekuwa namba mbili mara mbili. Hivyo ndivyo ilivyo. Unajua thamani ya urithi ilivyo? Hata Otamendi, Kevin de Bruyne, Fernandinho, Silva, Sterling, Aguero ni uwekezaji uliofanyika muda mrefu si miaka miwili iliyopita.
 
Hivi mnajua ni wachezaji wangapi wa Man United walibaki msimu uliopita? Walikuwa wanacheza wapi, walikuwa wanachezaje kama wanacheza. “Huo urithi wa Man United nilioukuta. Kocha ajaye wa Man United atakutana na Lukaku, Matic, De Gea na wengine bora atakaowatumia kwa muda mrefu, ambao wapo vizuri, timu na viwango bora kabisa. “Ukitazama robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, kuna timu nne. Barca, Real Madrid, Juve, Bayern wote hao wanafika hatua hiyo mara zote na, timu zao zipo vizuri.”
 
Back
Top Bottom