MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
Tuache tu mkuu...Kipi hicho?
Hapa tutaanza kuchambua mambo ya Uchumi, Kodi, Sheria na Morality.
Lakini kiufupi tu: Public Advertisement of Alcohol inawalakini mkubwa sana kwa watoto.
Uingereza, Ireland, Ufaransa na Urusi walifanya tafiti na kujua kwamba watoto wengi (Minors) walioona matangazo makubwa ya pombe wana hati hati ya kuanza kunywa pombe mapema kwenye Umri wao. Mwaka jana Ireland wameandaa hadi Muswada wa kuzuia matangazo ya pombe ili kulinda watoto. Wafaransa walivyofanya hivyo wamekuta utumiaji wa pombe kwa watoto umepungua kwa Asilimia 23% hivi ndani ya muda mfupi.
Sasa hapa ni lazima tujiulize kwamba,
Tukiwa tunazitoa hizo ofa kwenye vituo vya daladala Je tuna njia au mkakati wa kuwalinda watoto wetu wadogo wasipate hamasa ya pombe ??? Ndiyo maana nikasema tukianza kuyachambua haya mambo tutazungumzia Uchumi dhidi ya Morality.