Hivi mnajua ni wachezaji wangapi wa Man United walibaki msimu uliopita? Walikuwa wanacheza wapi, walikuwa wanachezaje kama wanacheza. “Huo urithi wa Man United nilioukuta. Kocha ajaye wa Man United atakutana na Lukaku, Matic, De Gea na wengine bora atakaowatumia kwa muda mrefu, ambao wapo vizuri, timu na viwango bora kabisa. “Ukitazama robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, kuna timu nne. Barca, Real Madrid, Juve, Bayern wote hao wanafika hatua hiyo mara zote na, timu zao zipo vizuri.”