Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ngono - ingawa cocaine huweza kutumika kama njia ya kuongeza hamu ya ngono huweza kusababisha kushindwa kumaliza kile ulichokianza. Matumizi sugu ya dawa hii ya kulevya huleta madhara kwa jinsia zote yani kwa wanaume na wanawake.
 
Moyo - Kwenye moyo huweza kuleta Shambulizi la moyo (heart attack) na vilevile mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio (Arrhythmia) hivyo unaweza kufa ghafla tu.
Kuna GIF hapa ya moyo inaonyesha mtu anayekufa kwa cocaine overdose dah! Madaktari nyie nawaheshimu [emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Nini hutokea baada ya matumizi ya muda mrefu ya kokeni?

Baada ya kutumia cocaine kwa muda mrefu punde unapoacha tu kutumia dalili zifuatazo hutokea;
Unyogovu
Uchovu
Kushindwa kuzingatia na kutokuwa makini
Kukosa uwezo wa kuwa na furaha au kusikia raha
Kuongezeka kwa tama zaidi ya kutumia cocaine
Kujisikia kuumwa, maumivu, baridi na kutetemeka.
 
Heroin
Hujulikana vilevile kama diamorphine, hutokana na mmea huitwao kitaalamu opium poppy. Heroin kwa mfumo wa Morphine hutumiwa hospitalini kama dawa ya maumivu makali ya ghafla (acute pain) kwenye maumivu makali ya kifua wakati wa shambulizi la moyo, na kwa maumivu ya mtu aliyepata ajali, vilevile baada ya upasuaji, na maumivu sugu kwenye kansa. Hivyo hutolewa kwa kuangalifu mkubwa.
 
Aina hii ya dawa ya kulevya huweza kutumika kwa kuvuta kwa pua, kuvuta kama sigara na kwa kuchoma kwenye mshipa. Siku hizi watu hutumia njia ya haja kubwa na kwenye uke, ambapo kuta hufyonza heroin na kuanza kufanya kazi ndani ya sekunde arobaini.
Heroin mara tu baada ya kuingia kwenye damu kuenda kwenye mfumo wa neva na kukandamiza ufanyaji kazi wake, ndio huweza kutumika kupunguza maumivu.
 
Nini madhara ya matumizi ya muda mrefu ya heroin?
Madhara ya matumizi ya muda mrefu wa dawa hii ya kulevya hutokana zaidi na matumizi ya sindano na vifaa vingine visivyo salama
Maambukizi kwenye kuta na milango ya moyo
Maambukizi ya ini na virusi (kama hepatitis C na HIV),
Maambukizi ya figo
Maambukizi ya mfumo wa hewa
Maambukizi ya ngozi na majip
 
KIJUE KILIMO CHA PAPRIKA : Paprika “Caspicum annum” ni mmea jamii ya pilipili isiyo kali, wengine, huiita pilipili tamu. Asili yake ni Amerika ya Kati. Tunda lake ni kubwa kuliko pilipili tuliyoizoea, refu na umbo la kuchongoka, aina nyingine huwa ya duara. Asili ya mmea huu ni bara la Amerika ya Kusini. Nchini Tanzania paprika inalimwa zaidi katika mikoa ya Iringa, Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha.
 

Attachments

Matumizi ya paprika ni pamoja na kutumiwa kama kikolezo cha asili kwenye mchuzi. Mbali na mapishi ya nyumbani, ambayo mara nyingi hutumia matunda yenye rangi ya kijani kibichi yasiyo komaa sana, paprika iliyokomaa kabisa hutumiwa sana katika viwanda vya kusindika aina mbalimbali za vyakula. Siku hizi watu wengi wanapendelea vyakula vyenye asili ya ogani, kuliko vya kemikali. Vilevile zao hili hutumiwa kwenye vipodozi na rangi za kupendeshea mwili. Kilishe, paprika ina virutubisho muhimu vya mwili, kama vitamini A na C, pamoja na madini ya chuma.
 
Dah!nawaza mbali sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…