Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna wakati gazeti la Kiu lilichapisha makala nzima nzima za kijasusi za The Bold. Mwenyewe alikuja kulalamika humu sana ila sidhani kama alipatiwa msaada wo wote. Baadaye hao Kiu nadhani walimlipa na alishauriwa kuwa makala hizo awe anaziwekea disclaimer kuwa ni mali yake na zisitumiwe nje ya JF bila ruhusa yake ya kimaandishi. Disclaimer hii ndiyo ingeweza angalau kumsaidia katika kupambana na plagiarists wa kazi zake. JF wenyewe nadhani wamekwepa jukumu hilo la kulinda contents za memba wake. Baadhi ya wanasheria pia walidai kuwa inakuwa vigumu kudai haki ya contents kisheria kwa sababu karibu kila mtu ni anonymous. Kwa hiyo, nijuavyo mimi, ukiweka kitu humu jua kuwa ni cha wote !!!
sahihi...humu unaweka mada kwa ajili ya 'matumizi ya wote'
 
Hapa naona pana shida kubwa dunia nzima,
Tukifika mahali tukasema tuache vitu tu kwasababu watu ni anonymous tutakuwa tunakosea sana.
Waandishi kama wakina George Orwell walikuwa wanatumia majina siyo yao wakaandika hadi The Animal Farm,
Lakini walilindwa saana: Nilikuwa nazungumza na Mkuu Consigliere siku moja, akaniambia kitu kizuri sana. Kwamba miaka 10 hadi 20 iyao Social Networks zinaweza kuja kuwa ndiyo vyombo vikubwa vya mawasiliano hapa duniani. Hivyo kama hatutajiandaa vizuri tutajikuta tunapelekwa na wimbo la mabadiliko bila kujiandaa (Hapa lazima tukubali wataalamu wetu wa Sheria na wadau mbali mbali wa mitandao wamelala sanaa) Duniani kwingine washaanza hadi mijadala ya kulinda hati miliki za mitandaoni na zile za makabila kama madawa ya Kienyeji nk.......

JF inaweza kuja kuwa mtandao mkubwa sana huko mbeleni, hasahasa ambavyo matumizi ya Mtandao yanaongezeka,
Tungetegemea kuona nayo iko mstari wa mbele kutafsiri mabadiliko ya dunia ya kisera za mitandao yana athari gani kwenye Uchumi wa nchi, Elimu na maisha ya watu kwa Ujumla. Privacy ipo lakini Malcom Lumumba wa JF ndiye yule yule Malcom Lumuba anayeshinda Ofisini akiandaa vitu mbali mbali, tofauti ni Alias tu...Sasa kwanini asilindwe ???

Kuna paper nzuri sana ya Semina kuhusu haya mambo ya kulinda hati miliki mtandaoni,
Nikipata wasaha ntakuwekea usome..........
 
IMG_20180323_124110_072.jpg
 
Back
Top Bottom