Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Gharama ya kudhibiti kupe kwa mwaka ni kubwa mno, inakisiwa kuwa shilingi za Kitanzania 8,400 hadi shilingi 18,000 kwa mnyama kwa mwaka. Kiasi hicho hutegemea aina ya dawa na njia itumiwayo katika kudhibiti. Mwaka 1997 ilikadiriwa kwa Tanzania kuwa hasara iliyotokana na kupe na magonjwa aenezayo ilifikia takribani shilingi bilioni 77 kwa mwaka, kati ya hasara hiyo Ndigana kali vilichangia upotevu wa zaidi ya shilingi bilioni 42 na kupunguza uzalishaji wa maziwa ulipungua sana. Upungufu uliokadiriwa kusababisha hasara wa shilingi bilioni 7 na milioni 560 (7,560,000).