Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

hehehe kwann ufikirie hvyo, hakuna kufikiria hvyo
Hata maandiko yanasema wanandoa yawapasa kupendana na kuvumiliana katika shida na raha. Usifurahie raha unazozipata tu, fikiria pia je, huyu mwenza wangu siku akiwa tofauti na hivi nimfurahiavyo ntaendelea kumpenda na kumfurahia???

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Kama wanandoa wataweza kuvumiliana katika hali zote hizi basi wataishi kwa furah kwa sababu watakuwa wamezipitia nyakati zote hizi, hivyo kila mmoja atamuona mwenzake ni muhimu zaidi.
 
9. Muwazie mema mke au mume wako.
Ndoa nyingi zimekuwa zikifurahia maisha ya ndoa kwa sababu wote wanawaziana mema. Mhurumie umpendaye, mjali mtie nguvu pale ambapo anakata tama, weka upendo wako wote kwake.
 
Ambaye kapata likes zaidi ya kumi kwenye post yake kupitia thread hii aitupie [emoji1] [emoji1] [emoji1]
IMG_20180325_112623.jpg
 
Siri 6 Muhimu Zinazofanya Mahusiano Kudumu Katika Hali Ngumu
Labda nianze kwa kusema kuwa ndoa nyingi ama mahusiano mara nyingi yana migogoro na hii ni hali ngumu sana ambapo ndoa/mahusiano hupitia. Zipo ndoa ambazo hupata hali ngumu na kufikia kuachana kabisa eti kwasababu ya uchumi, Hapa pana njia kadhaa zitakazo epusha haya yasitokee.
 
1. TAMBUA NA FANYIA KAZI TATIZO.
Wakati joto la tatizo limepanda sio wakati wa kuwa na hasira juu ya mwenzi wako. Unapokuwa na matatizo, na hata kukusababisha shinikizo la damu kwako na saa fulani unakosa mwelekeo.
 
Na hii inasababisha kutoelewana na mtu yeyote karibu yako, na pia unaanza kujitenga na kuwa peke yako, lakini yakupasa kugeuka na kumwambia mwenzi wako kuwa “ angalia tupo katika hali ngumu, na kuishugulikia hii hali wote kwa pamoja.
 
2. Tambua mambo yanayokufanya kuwa na misongo katika uhusiano wako.
Kwa uzoefu tu, hata taifa huwa linaporomoka kiuchumi pia, hivyo inakupasa kumbuka kuwa tatizo si mwenzi wako, bali kutokuwepo na utunzaji mzuri wa mshaara, au kukosa kazi na hata pia uwepo wa madeni mengi. Hivyo yakupasa kuelekeza shabaha yako mahali pazuri.
 
Kwasababu ukishagundua tatizo ni vyema kujaribu kushirkiana kwa pamoja katika kutatua tatizo kwa kutoa njia sahihi zitakazotumika kutatua tatizo.
 
3. Kuwa mkweli katika hisia zako.
Mawasiliano mazuri yenye uhakika chanzo chake ni ukweli na kuwa wazi. Kama umeaga kuwa unaenda kutafuta kazi sehemu fulani basi fanya ulichokipeleka. Usiseme kuwa unakwenda kutafuta kazi huku humanishi hivyo. Kuwa tu muwazi kwa kila kitu huku ukiruhusu mambo mengine kutoka kwa mwenzako.
 
Back
Top Bottom