Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jina la kwanza la Google lilikua backrub
Google hukodisha Mbuzi kwaajili ya Kukata Majani nje ya Ofisi zake
Pengine unge hisi kwa kuwa Google ni kampuni tajiri sana basi lazima kuna watu wa kutunza na kukuta majani ya kwenye Garden za nje ya ofisi yake lakini, Kama sehemu ya kutunza mazingira, kampuni ya Google hutumia wanyama mbuzi kukata majani nje ya ofisi zake.
 
852236492_135651.jpg
 
Google ilikua inahifadhiwa kwenye Hard Disk yenye ukubwa wa GB 4
Hapo zamani GB 1 ilikua ikionekana kama ndio memory kubwa sana kiasi kwamba huduma zote za Google pamoja na Tovuti yake ilikuwa ikihifadhiwa kwenye Server yenye ukubwa wa GB 4, Kingine cha kushangaza ni kuwa Server hiyo ilikuwa imetengenezwa kwa toi za kuchezea watoto maarufu kama LEGO.
 
Google ina miliki kikoa hichi “466453.com” sababu ndio hizi
Google ina miliki vikoa (domain) kadhaa ambazo zimekosewa lakini zina maana ya Google, kwa mfano google inamiliki vikoa vilivyokosewa vya Gooogle.com, Gogle.com, Googlr.com zote zikiwa kwa matamshi zina maana ya neno Google. Kuhusu kikoa cha 466453.com google ina miliki kikoa hichi kutokana na namba hizo kwenye keyboard ya simu yako ya tochi zina maana ya neno “Google”.
 
Google ina miliki kikoa hichi “466453.com” sababu ndio hizi
Google ina miliki vikoa (domain) kadhaa ambazo zimekosewa lakini zina maana ya Google, kwa mfano google inamiliki vikoa vilivyokosewa vya Gooogle.com, Gogle.com, Googlr.com zote zikiwa kwa matamshi zina maana ya neno Google. Kuhusu kikoa cha 466453.com google ina miliki kikoa hichi kutokana na namba hizo kwenye keyboard ya simu yako ya tochi zina maana ya neno “Google”.
 
Jina la Samsung Lina Maana ya Nyota Tatu
Nchini korea maana ya neno Samsung ni nyota tatu kwa kiswahili, mwanzilishi wa kampuni hii aliamua kuja na jina hili baada ya kuwa na ndoto ya kufanya kampuni hiyo kuwa kubwa na juu zaidi kama nyota. Ndio maana logo ya kwanza ya kampuni hiyo ina nyota tatu.
 
Logo ya Samsung Imebadilishwa Mara tatu tu
Ni kawaida sana kwa makampuni kufanya mabadiliko mbalimbali, hii inaweza ikawa mabadiliko ya kibiashara au hata mabadiliko ya muonekano lakini kwa samsung hili ni tofauti kidogo kampuni hii haijafanya mabadiliko makubwa sana ya kimuonekano kwani kampuni hii toka kuanzishwa kwake mwaka 1938 imefanya mabadiliko ya logo yake mara tatu tu tofauti na kampuni nyingia ambazo tunazijua sasa. Logo inayotumika sasa ilianza kutumika rasmi mwaka 1993.
 
Bidhaa ya kwanza ya Kieletroniki kutoka Samsung ni TV
Kwa sasa samsung inajulikana sana kwa utengenezaji wa vitu mbalimbali vya kieletorniki, lakini miaka ya nyuma kabla ya utengenezaji wa vifaa hivyo samsung ilikua ikifanya biashara ya usindikaji wa chakula, biashara ya nguo, bima, ulinzi na biashara nyingine za rejareja. Kufikia miaka ya 1960 kampuni hiyo ilingia kwenye biashara ya vifaa vya kielectroniki na ndipo mwaka 1970 kampuni hiyo ilifanikiwa kutoa bidhaa ya kwanza ambayo ilikua ni TV yenye rangi mbili tu nyeusi na nyeupe.
 
Jengo Refu kuliko Yote Duniani la Burj Khalifa Limejengwa na Samsung
Najua utakuwa umeshtuka kidogo lakini ni kweli, Kampuni ya samsung inajumuisha makampuni zaidi ya 80 ambayo yanafanya kazi mbalimbali ikiwemo kazi ya ujenzi. Kampuni ya Samsung C&T Ndio iliyokuwa mjenzi mkuu wa jengo hilo refu kuliko yote la Burj Khalifa ambalo lipo nchini Dubai. Hata hivyo Samsung ilishirikiana na makampuni mengine kujenga gorofa hilo.
 
Back
Top Bottom