Bidhaa ya kwanza ya Kieletroniki kutoka Samsung ni TV
Kwa sasa samsung inajulikana sana kwa utengenezaji wa vitu mbalimbali vya kieletorniki, lakini miaka ya nyuma kabla ya utengenezaji wa vifaa hivyo samsung ilikua ikifanya biashara ya usindikaji wa chakula, biashara ya nguo, bima, ulinzi na biashara nyingine za rejareja. Kufikia miaka ya 1960 kampuni hiyo ilingia kwenye biashara ya vifaa vya kielectroniki na ndipo mwaka 1970 kampuni hiyo ilifanikiwa kutoa bidhaa ya kwanza ambayo ilikua ni TV yenye rangi mbili tu nyeusi na nyeupe.