Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni kweli kuwa kwa watu wengine kuchora ni kipaji lakini kama wewe ni kama mimi na kuchora kwako ni mthiani basi jaribu App hii mpya ya SketchAR. App hii inakupa uwezo wa kipekee kuweza kujifunza kuchora na ni rahisi sana kuitumia na huitaji ujuzi wowote zaidi ya kuwa na smartphone yako.
 
Kwa kutumia mfumo wa AR au Augmented Reality, App hii itakusaidia kuweza kuchora kwenye karatasi kwa kufuata hatua chache, Kwanza unachotakiwa kufanya ni kuchora vidoti vya duara kwenye karatasi yako kisha chukua simu yako na washa App ya SketchAR kisha chagua mchoro na nyooshea kamera yako kwenye karatasi zenye vidoti hivyo vya duara.
 
Kitakacho tokea ndani ya App hiyo kutatokea mchoro ambao utakuwa juu ya karatasi yako, mchoro huo utaonekana ndani ya kioo cha simu yako kisha unatakiwa kufuatiliza vipengele kwa vipengele jinsi App hiyo itakavyo kuwa ikikupa maelekezo. Njia hii ni rahisi na unaweza kujifunza kuchora kwa urahisi kwa kufanya mazoezi ya kila siku.
 
Back
Top Bottom