Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Miili yetu ina umeme au nguvu ambayo inaizunguka. Nguvu hiyo inategemeana na Afya, Hisia, Mawazo, na kila wakati hubadilika badilika kutegemea na hali iliyopo katika mwili. Ni suala la kisayansi na sio la kufikirika. Miili yetu imezungukwa na energy ambayo ipo katika mawimbi mbalimbali yanayotegemeana na hali ya mwili ilivyo. Mfano mwili wenye afya mawimbi yake ya energy au nguvu kani yapo tofauti na mwili ambao hauna afya, vilevile mwili wenye hisia au fikra fulani nao pia una mawimbi yake ambayo nayo hutegemeana na hisia iliyopo.
 
Kwenye hali ya furaha kuna aina ya mawimbi yanakuzunguka na kwenye hali ya wasiwasi au kwenye hali ya kuwa na wazo lolote baya au hali yoyote mbaya nayo inabadilisha nguvu ya mwili inayokuzunguka. Kazi ya nguvu hii ni kulinda mwili na kusambaza ujumbe katika hali ya mawimbi kwenye kila kona ya mwili.
 
Mtu mwenye kuumwa mfano kansa ana mawimbi yanayomzunguka 42Hz au zaidi na ukiwa na mawazo au fikra hasi unakuwa unapunguza mawimbi -12Hz na ukiwa na mawazo chanya unakuwa umeongeza mawimbi +10Hz. Hivyo mawimbi yetu yanachangiwa na hali ya miili yetu pamoja na hali ya Akili na ufahamu wetu.

Ni kwanini watu wengi hushikiliwa mawazo yao hasa mawazo mabaya badala ya kushikilia mawazo mazuri?
 
Umeshawahi kuongea na nafsi yako kibinafsi? Umeshawahi kujaribu kuchunguza kinachoendelea akilini mwako? Mfano kuchunguza unawaza nini? Kuna wakati unakuta unawaza mawazo mabaya na unaweza ukajisemea mwenyewe "Acha kuwaza mawazo mabaya, hayana umuhimu" huku ukijiambia mwenyewe.Unaweza kuwa makini na mawazo yako na kuyauliza kama unavyouliza mtu mwingine au kuyachunguza kama unavyochunguza hali ya nje.
 
Kushindwa Kuwa makini na Jambo.
Tunaposhindwa kuelewa jambo kwa kina wengi hujikuta wanaweka fikra duni na kushikiliwa na mawazo hasi. Tunaposhindwa kuelewa hali iliyopo basi tunaweza kuzidi kutawaliwa na wasiwasi, hasira, ujinga n.k lakini tukielewa jambo au hali kwa uhalisia wa pande zote mbili yaani kwa upande unaotetea na upande unaopinga au kwa upande hasi na upande chanya tunaweza kufanya maamuzi sahihi na kutoshikiliwa na mawazo bila kujiongoza.
 
Badili wazo au Fikra mbaya kwa Kuipa Fikra nzuri/chanya kipaumbele.
Huwezi kuondoa mawazo au fikra mbaya kwa fikra mbaya bali vyote hivyo huondolewa kwa fikra nzuri. Mfano unapoona hasira inakutawala, ili kuiondoa hasira weka mtazamo wako kwenye upendo na hasira yenyewe itaondoka bila kipingamizi. Ibadili hasira kwa kutanguliza upendo na hasira yenyewe itaondoka kwani hakuna upendo unaokaa na hasira. Kama vile hakuna giza linalokaa na mwanga ndivyo hakuna mawazo au fikra mbaya inayoweza kukaa na fikra nzuri. Fikra nzuri huondoa fikra mbaya na mawazo mazuri huyaondoa mawazo mabaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…