Avartar yako inabambaHahahaha!
Wengi wanapoamka asubuhi kuanza kujiandaa na shughuli zao mbalimbali. Mfano kama ni mwanafunzi anajiandaa kwenda shule na kama ni mfanyakazi naye anajiandaa kwenda kazini.
Wengi wanapoamka asubuhi kuanza kujiandaa na shughuli zao mbalimbali. Mfano kama ni mwanafunzi anajiandaa kwenda shule na kama ni mfanyakazi naye anajiandaa kwenda kazini.
Mzunguko huu huishia pale mtu anaporudi nyumbani, anapumzika labda kwa kutazama Television, au anasikiliza redio, au unaposhiriki maongezi mbalimbali na mwisho siku inaisha unapolala. Gurudumu hili litaendelea hapo kesho yake na kama siku ya kesho ni tofauti labda ni siku ya weekend basi kunakuwa na gurudumu lingine la mfumo wa kuifanya siku ipite.
Je unatenga muda wa kuweza kujitafakari?
Wengi wanatumia siku yao kujituma, kufanya majukumu yao, kushirikiana na wengine n.k lakini ni wachache sana ambao hutumia muda fulani maalumu kwa lengo la kujitafakari.
Inapaswa kutenga muda ambao utakuwa huru, hautaingiliwa na mtu katika mazungumzo ya muda mrefu, au hautapata usumbufu wowote. Muda huu utakuwa unajitafakari vyema. Unaweza ukawa unajitafakari kwa;
Kutafakari siku ilivyoenda/inavyoenda,
Kutumia nafasi kupumzisha akili,
Kujitafakari
Makamanda watasema hilo pango ni CCM [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Sorry kuingiza matani ya siasa lakini uko sahihi. Tasnifu za uzamivu maelfu zimeshaandikwa kuhusu Allegory hii na kila mmoja anasema lwake japo wengi wanaamini kuwa pengine Plato alikuwa anaongelea maisha na/au maarifa. Kuna watu wanaoamini kuwa maisha haya tunayoishi ni kivuli tu cha uhalisia wenyewe. Maarifa hali kadhalika. Ati, ni kweli tunajua tukijuacho au tukijuacho ni mwanga hafifu tu wa kile tunachopaswa kukijua? Yawezekana wote tuko pangoni.....MAANA.
Mpaka leo limebaki kuwa ni fumbo japokuwa wengi wamekuwa wakijaribu kutafsiri Plato alikuwa anamaanisha nini alipokuwa akielezea uhalisia wa mwanadamu. Fumbo hilo kila mmoja anaweza kulifikiria kivyake na kujitahidi kujitoa katika pango na kuweza kujitambua zaidi.