UNAWEZA KUWA NA FURAHA PALE UNAPOAMUA KUWA NA FURAHA, KWANI FURAHA NI MTAZAMO WA MTU NA SIO UHALISIA KAMILI”
Umeshawahi kujiuliza furaha maana yake ni nini? Inaweza ikawa na maana tofauti kwa watu tofauti mfano, wapo wanaoona furaha ni pesa, wengine huona furaha ni kutenda mema, wengine hutafsiri furaha ni raha, urembo au chochote ambacho wanaona kinawapa furaha. Lakini ukweli ni kuwa, furaha ni fikra. Unaweza kuwa na furaha pale unapoamua kuwa na furaha hata kama mazingira na hali iliyokuzunguka inakupa huzuni. Angalia katika maisha yako, shukuru kwa kila jambo na weka mtazamo chanya katika mawazo na fikra zako.