Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NAFASI YA KUPANDA:

Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita
 
PALIZI:

Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na

maguguyanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi minne ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa namagugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu
 
Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.

Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.

Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.
 
UVUNAJI:

Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.
 
USINDIKAJI BORA
Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:

- Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji

- Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo

- Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.
 
Njia bora za usindikaji

- Kwa kutumia mashine aina ya Grater

Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
 
MATUMIZI YA MUHOGO
Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
- Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga

wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k

Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.
 
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU


Kuna magonjwa mawili ambayo ni muhimu sana na yanapunguza uzalishaji wa zao la muhogo.
a) Ugonjwa wa Matekenya au Ugonjwa wa michirizi ya kahawi katika muhogo
Ugonjwa huu ni maarufu kwenye sehemu zenye miinuko iliyo na urefu chini ya mita 300 na unapatikana kidogo sana kwenye miinuko ya mita 500 na kuendelea ambako uenezaji wake wa kawaida hautokei kabisa.
 
Dalili za Ugonjwa
Sehemui zote za muhogo zinaweza kuonyesha dalili za uambukizo wa ugonjwa huu lakini ni vipengele gani vya ugonjwa na ni kwa kiwango gani hutegemea hali ya mzingira, hatua ya kukua kwa mmea kwa kulinganisha.
 
Back
Top Bottom