Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

67cb9dfb-957c-4aec-80ce-dc243222672b.jpg
 
Timu ya Manchester City imenoa silaha zake jana Jumatatu jioni katika mazoezi yake kabla ya kuikabili Liverpool kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya unaotarajiwa kupigwa kesho Jumatano usiku.
Kikosi cha Pep Guardiola kinahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa taji Ligi Kuu England.
Barani Ulaya macho ya mashabiki wa soka macho yote yataigeukia mechi hiyo ili kuipa nafasi timu itakayoibuka na ushindi kutinga nusu fainali ya msahindano hayo.
Man City inaingia kifua mbele katika mechi hiyo kesho ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wake wa mwishoni mwa wiki baada ya kuifunga Everton kwa mabao 3-1.
Timu hiyo ya Etihad itashuka uwanjani akili yake ikiwa imeelekeza kwa nyota Kevin De Bruyne na Sergio Aguero wakisaidiana na Raheem Sterling, Bernardo Silva na Gabriel Jesus.
 
BEKI wa kati wa Bayern Munich, Mats Hummels amekiri amekuwa mwenye furaha kubwa baada ya timu yao kuikwepa Liverpool kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Miamba hiyo ya Ujerumani na badala yake sasa itavaana na Sevilla, huku Liverpool ikiwa na kibarua na Waingereza wenzao, Manchester City katika hatua hiyo ya nane bora, ambaye anayepigwa basi anafungasha virago.

Hummels aliwahi kuwa chini ya Kocha Jurgen Klopp, anayeinoa Liverpool kwa sasa, hivyo anafahamu wazi mbinu za kocha huyo anapokuwa kwenye mechi kama hizo kwa sababu alikuwa moto Borussia Dortmund.

“Nafahamu timu za Klopp nguvu yake,” alisema Hummels.

“Nafahamu timu yake inavyokuwa nzuri kupita kiasi inapofikia hatua kama hii. Wakati mwingine inakuwa vigumu sana kucheza na timu ambazo zipo kwenye nafasi za chini kwa misimamo ya ligi zao.

Liverpool ni timu ambayo siku zote inacheza mpira mkubwa sana inapokutana na timu bora.

“Ukweli sidhani kama kuna timu zilizobaki kwenye hatua hii zingependa kukutana na Liverpool. Shughuli yao ya uwanjani si ya kitoto, wasumbufu na inawachezaji wenye viwango, hasa kwenye fowadi yao.”

Liverpool imefunga mabao 28 katika mechi nane ilizocheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu hadi kufikia katua iliyofikia kwa sasa ya robo fainali, ambapo kesho Jumatano itakipiga na Man City huko Anfield.
 
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema anaamini kikosi chake kitaibuka na ushindi mnono mbele ya Juventus katika mechi ya robo fainali inayotarajiwa kupigwa leo Jumanne usiku.
Kikosi cha Real Madrid kitashuka kwenye dimba la Allianz Arena kwa ajili ya mchezo huo wenye presha kubwa kwa makocha na mashabiki kulingana na historia ya timu hizo kila zinapokutana.
 
Mechi hiyo inampa wakati mgumu zaidi kocha Zidane ambaye anatajwa kuwa kwenye orodha ya makocha ambao siku za usoni huenda wakainoa Juventus. Lakini upande wa pili anakabiliwa na presha kubwa ya kutetea taji hilo la Mabingwa Ulaya msimu huu.
 
Zidane ambaye amewahi kuitumikia Juventus akiichezea kwa miaka mitano, ana kibarua kigumu mbele ya wababe hao wa Italia ambao anawajua vyema mfumo wa uchezaji wao.
Kocha huyo pia alizungumzia suala la Max Allegri ambaye anatajwa kuwa kwenye mbio za kumrithi Antonio Conte. Huku akisema kwamba kwa sasa anafurahia maisha Real Madrid ikifika wakati akawa sehemu nyingine basi hawezi kupingana na hali hiyo.
 
SUPASTAA Pierre-Emerick Aubameyang hana hata siku nyingi kwenye kikosi cha Arsenal. Amecheza mechi sita tu za Ligi Kuu England tangu atue hapo, lakini tayari ameweka jina lake kwenye historia ya klabu hiyo yenye maskani yake Emirates.

Staa huyo juzi tu hapo, alipiga mbili wakati kikosi hicho cha Arsene Wenger kilipotembeza kipigo cha Bao Tatu Bila dhidi ya Stoke City kwenye mchakamchaka wa Ligi Kuu England.
 
Aubameyang kwanza alifunga kwa mkwaju wa penalti kabla ya kutupia wavuni bao jingine kwa mpira alioupiga kwenye engo ambayo kipa wa Stoke, Jack Butland hakuwa na maajabu ya kuuzuia.

Staa huyo wa Gabon alikuwa na nafasi ya kupiga ‘hat-trick’ baada ya Arsenal kupata penalti nyingine, lakini badala yake aliona sio ishu na kuamua kumpa straika mwenzake, Alexandre Lacazette, ambaye alikuwa hajafunga siku nyingi, naye atoe ukame. Lacazette akatia kambani penalti hiyo.
 
Licha ya uamuzi huo wa Aubameyang, bado anakuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwa wachezaji wote waliowahi kuichezea Arsenal na kufunga katika mechi zao sita za kwanza.

Auba kwa sasa amefunga mabao matano katika mechi sita za kwanza alizocheza kwenye Ligi Kuu England akiwa na jezi za Arsenal. Shida kwa Arsenal hawawezi kumchezesha mechi za Europa na keshokutwa itakipiga na CSKA Moscow, robo fainali ya kwanza huko Emirates.
 
At funerals
Other countries; we've lost a good friend
My country; mschew hata hiyo mchele haijawekwa chumvi vizuri
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Americans; when I look in your eyes I see my happiness
Kenyans; Ushaiguzwa pahali ukaskia kukojoa?
Nn mbaya na nyinyi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
A baby is not a mistake or a surprise...You had sex without a condom! Right??what did you expect A flat screen TV[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom