Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Staa wa filamu Riyama Ally amesema hakujachukia kukosa tuzo kwani hakupeleka muvi yake ya aina yoyote katika kinyang'anyiro cha Tuzo za Sinema Zetu.

Hivyo amefunguka na kusema watu wasimuandame kwa kumwambia amechukia Wema Sepetu kupata tuzo hiyo.

Riyama amesema hayo baada ya watu wa mitandaoni kumsakama kuwa amechukia kwa kitendo cha Wema kupata tuzo ya muigizaji bora wa kike ambayo katika kipengele hicho Riyama naye aliwekwa kuwania hiyo.
 
Mie nashangaa watu wanaonisakama kuwa nimechukia kukosa tuzo, sasa mimi nichukie nini wakati hata sijapeleka muvi yangu yoyote? Nashindwa kuwaelewa watu hao, halafu siwezi mchukia Wema kisa kapata tuzo kwani yeye ni nani hadi akose Tunzo? Watu wache maneno ya kusemeana," alisema Riyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…