Hivi aliyeanza personal attack kati yake na mimi ni nani!? Kwa mamlaka gani aliyokuwa nayo humu ya kunizuia kuandika kile nikitakacho kuandika? Umeona aliniambia get help? Nipate msaada kwa lipi hasa!?
Kama kuna mtu hapendi ninachoandika humu tushindane kwa hoja siyo kutaka kunizuia kile nilichoandika au kuniambia nitafute msaada. Sihitaji msaada wowote ule.
Hayo ya awamu zilizopita yazungumziwe pia na awamu hii. Sijawahi kumzuia yeyote humu kuandika kuhusu awamu ya Baba wa Taifa au awamu yeyote ile na mimi hakuna mwenye haki ya kunizuia kuandika ya awamu hii. Ukinishambulia namna yoyote ile kutaka kuonyesha mimi nina matatizo katika kukemea maovu, udhalimu na dhuluma za awamu hii basi narudisha mapigo.
Mkuki ukiwa mchungu kwa nguruwe basi uwe mchungu pia kwa binadamu.