Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Steven Gerrard, shujaa wa Liverpool katika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya AC Milan mwaka 2005 alidai wachezaji wa Liverpool walionyesha ubora wao katika mambo mawili, ukabaji na ushambuliaji.

“Nadhani tumeziona pande zote mbili za Liverpool leo, jinsi walivyoshambulia kwa kasi wakati wakiwa na mpira, pia kuutafuta na kuupata. Katika kipindi cha pili walikuwa bora katika kumkaba mtu mmoja mmoja na waliwalazimisha City kutokuwa na mipango,” alisema Gerrard.
 
Wakati Gerrard akisema hayo, staa wa zamani wa Manchester United, Roy Keane aliiponda vibaya City akidai wamekuwa wakipewa sifa nyingi zilizopitiliza.

“Itakuwa mechi ngumu kuichambua. Baada ya mechi Kocha (Pep Guardiola) alisema walikuwa wamemiliki sana mpira, lakini umiliki wa mpira haukuwezeshi kushinda mechi. Kumekuwa na sifa nyingi ambazo hii timu ya City inapewa. Kuna sifa wao ni timu kubwa. Leo wamepewa angalizo,” alisema Keane.
 
Wana mambo mengi ya kufanya kabla ya kufikiriwa kuambiwa wao ni timu kubwa. Ulikuwa ukiwaangalia wachezaji wa City ni wazi walikuwa wanashangazwa sana na kilichokuwa kinaendelea. Kulikuwa hakuna namna ambavyo walikuwa wanaona wangeweza kupigwa 3-0.”
 
Ingawa walikuwa wanajua utakuwa ni usiku mgumu lakini walikuwa na uhakika wangefunga bao kwa hiyo walishtuka sana. Nadhani kwa tulichokiona msimu huu walionyesha ukosefu wa ubora lakini inabidi uwapongeze Liverpool kwa hilo,” aliongeza Keane.
 
Katika mchezo huo, City ilishindwa kupiga shuti lililolenga lango hata moja katika lango la Liverpool. Hii ni mara yao ya kwanza kumaliza mechi bila ya kupiga shuti tangu Oktoba 2016.
 
Noleji ni Nguvu
IMG_20180406_210554.jpg
 
[emoji124] [emoji124] [emoji124] nakupita kama sijakuona vile. Baki na swali lako
[emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji3][emoji16][emoji16][emoji16][emoji3][emoji16][emoji3][emoji16][emoji3][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji16][emoji3][emoji3][emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji16][emoji3][emoji3][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom