Ugonjwa wa Baridi Yabisi ni Nini?
Ugonjwa wa baridi yabisi ni ugonjwa ambao unaathiri membreni ya sinovio na tishu inayozunguka vifundo (jointi); tishu hizo huwa nene, huganda kwenye kifundo na huharibu na kulemaza kifundo husika. Ukiachwa bila kutibiwa, ugonjwa huu unaweza kuharibu vifundo vibaya kiasi kwamba havitafanya kazi tena. Ugonjwa huu unapatikana mara nyingi kwa wanawake wanaoanza kuwa watu wazima hadi wenye umri wa kati. Ili kutambua ugonjwa huu, daktari wako atakuchunguza, atachukua picha ya X-ray na vipimo vya damu vinaweza pia vikahitajika.