Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Capturekho.PNG
 
Fuata Mtindo wa Maisha Yenye Afya

Wakati hakuna hata mmoja anayejua sababu za ugonjwa wa baridi yabisi, vidokezi hivi vinaweza kukusaidia kupunguza dalili zako.

1. Tafuta uwiano sawia wa mapumziko na kazi.

2. Jifunze njia za kupunguza au kutawala msongo.

3. Waombe wanafamilia au marafiki kukusaidia kazi.

4. Bakia kwenye uzito wako sahihi.
 
Tumia Vifaa Maalumu

Hata kazi rahisi zinaweza zikawa ngumu kufanya vifundo vyako vinauma. Vifaa maalumu na visaidizi vilivyo orodheshwa hapa vinaweza kurahisisha mambo kwa kupunguza mkazo na kulinda viungo. Mwulize mhudumu wako wa afya ni wapi unaweza kupata vitu hivi na vifaa vingine vinavyosaidia:
 
Vitu vya kuokotea na kushikilia vyenye mpini mrefu.

2. Vifaa vya kufungulia gudulia na kutungia nyuzi.

3. Banzi au vijiti kwa ajili ya kifundo vya mikono ya mbele na vifundo vingine.

4. Vitu vikubwa vya kushikia, penseli, vifaa vya bustani na vifaa vingine vinavyoshikwa kwa mkono.
 
Anza Kufanya Mazoezi

Mazoezi ya taratibu yanaweza yakafanya iwe rahisi zaidi kutumia vifundo vyako. Zingatia mambo yafuatayo wakati unapofanya kazi nje:

1. Chagua mazoezi yanayoimarisha mjongeo wa vifundo na kufanya misuli yako iwe na nguvu zaidi. Daktari wako au mtaalamu wa mazoezi ya viungo anaweza kukupendekezea mazoezi mengine.
 
Shughuli zenye athari ndogo kama vile kutembea, kuendesha baiskeli au kufanya mazoezi kwenye maji ya uvuguvugu, ni zenye kufaa.

3. Usijilazimishe kwa nguvu mno unapoanza. Jenga ustahimilivu wako taratibu kwa kipindi Fulani.

4. Wakati hali ya maumivu na kukakamaa ni mbaya sana, punguza kazi zako.
 
Tiba ya Dawa Inaweza Kusaidia

Madawa hayawezi kuponyesha ugonjwa wa baridi yabisi, bali yanaweza kukusaidia ujisikie vizuri zaidi. Wakati mwingine zinaweza hata kukomesha ugonjwa, daktari wako anaweza kukuandikia dawa moja au zaidi kati ya hizo. Hakikisha unazitumia kama ilivyoelekezwa. Zinasaidia sana kwa kuzuia uharibifu wa vifundo kama zitaanzishwa mapema wakati wa ugonjwa.
 
Vidokezi vya Kutumia Dawa

Daktari wako anaweza kurekebisha aina ya dozi ya dawa zako kulingana na hitaji. Kwa matokeo mazuri fuata vidokezi hivi:

1. Tunza orodha ya madawa yako yote. Mweleze orodha hii kila daktari unayeonana naye.

2. Tumia madawa yako kama ulivyoelekezwa tu.

3. usiruke wala usiache kutumia dawa bila kuzungumza na daktari wako.

4. Tafuta kujua kama dawa zako lazima zitumiwe pamoja na chakula.

5. Mwambie daktari wako kama umepatwa na athari kama kizunguzungu na matatizo ya tumbo.
 
Fanya vipimo vyote vya maabara ambavyo umeagizwa na daktari wako. Matokeo haya yatamsaidia daktari wako kufuatilia namna ambavyo dawa zako zinakuathiri.

Kama Upasuaji Unahitajika

Kwa watu wenye uharibifu mkubwa wa vifundo (jointi), upasuaji unaweza ukapunguza maumivu na kufanya iwe rahisi kutumia kiungo. Kwa kawaida kubadilisha kifundo, hasa cha nyonga au goti, ndio ambazo zinafanyiwa mara nyingi upasuaji katika hali hii. Aina nyingine za upasuaji zinaweza kufanyika ili kusaidia kusaidia kuzuia matatizo mikononi au miguuni
 
Back
Top Bottom