Ugonjwa wa baridi yabisi ni tatizo linalojulikana na ambalo huathiri ubora wa maisha wa takribani theluthi moja ya wanaume na wanawake . Mungu ametuahidi kwamba “…………watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mbawa kama tai, watapiga mbio wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu wala hawatazimia.” (Isa 40:31). Mungu akusaidie kuishi maisha ya afya na mtindo wa maisha wenye uwiano sawa, na uepuke kukakamaa kwa viungo na maumivu.