Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hubeba mimba ndani ya miezi kumi na tano, na huzaa mtoto mmoja baada ya kipindi hicho, twiga hujifungua akiwa amesimama tuu, na huzaa mtoto mrefu sana, mtoto ambaye huwa na kilo zaidi ya 50, ndani ya saa kadhaa mtoto wa twiga huanza kufanya mazoezi ya kukimbia, katika kipindi hiki mama huwa mlinzi mzuri wa mwanaye.
 
Inasadikika nyama ya kiumbe huyu ni tamu pasina mfano, laiti kama uhifadhi usingekuwepo basi wanyama hawa wangekuwa walishakwisha, katika kuthibitisha hilo si binadamu tuu bali karibia wanyama wote walao nyama humuwinda twiga kwa udi na uvumba, na kwakuwa mkubwa hakamatiki basi wanyama hao huwawinda watoto wa twiga tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…