Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jumapili hii mji wa Gold Coast Australia utaukabidhi kijiti cha uenyeji wa michezo ya jumuiya ya madola mji wa Birmingham wa Uingereza.
Birmingham inategemea kuwa mwenyeji wa michuano ya jumuiya ya madola ya mwaka 2022.
Mpango wa paundi milioni 70 kukipanua na kukiboresha Alexander Stadium ya Birmingam umetangazwa.Mpango huo utakiboresha kiwanja hicho chenye umri wa Zaidi ya miaka 40 kutoka kuweza kubeba watu 12,700 mpaka watu 40,000.
 
[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
446330984_41896.jpg
 
Tayari picha ya namna kiwanja hicho kinavyotarajiwa kuonekana imewekwa wazi na iwapo mpango utasalia ulivyo basi nchi nyingi zitaweza kuziona rangi za bendera zao kwani paa la Uwanja huo litakuwa na mifuniko ambayo ina rangi za bendera za nchi kadhaa Duniani.
 
Goli la penalti lilofungwa na Cristiano Ronaldo katika dakika za majeruhi limeiingiza Real Madrid katika nusu fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Penati hiyo ilikuja baada ya Medhi Benatia katika mazingira yenye utata kumdondosha Lukas Vazquez kwenye eneo la hatari.
Ni katika mazingira hayo hayo, kwa kile kilichosemwa kuwa ni matumizi ya lugha mbaya, mlinda mlango wa Juve, Gianluigi Buffon katika ile ambayo inaweza kuwa Champions League yake ya mwisho alitupwa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi muingereza Michael Oliver
 
Real, washindi mara tatu wa Ligi ya mabingwa Ulaya katika misimu minne, waliingia katika mechi hiyo ya mzunguko wa pili wakiongoza kwa mabao 3-0 lakini viongozi hao wa Seria A walianza kupoteza matumaini pale Mario Mandzukic aliposukuma kichwa nyavuni kutoka kwenye mkwaju ulionyunyizwa na Sami Khedira dakika mbili tu tangu kuanza kwa mchezo.
Huyo huyo Mandzukic akapata goli la pili kupitia kichwa muda mfupi kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza.
Blaise Matuidi akafunga la tatu kutokana na makosa yaliyofanywa na Keylor Navas na hivyo kuifanya Juventus iwe na matokeo sawa na Real Madrid, jambo ambalo lingeipeleka mechi katika dakika za nyongeza kama siyo tukio la Penati lililotokea na kuifanya Real Madrid kutinga nusu fainali katika mazingira ambayo mashabiki wao walikuwa tayari wamekata tamaa.
 
Sasa, Real inaungana na Liverpool, Roma na Bayern katika droo ya timu nne zilizosalia, droo itakayofanyika Nyon, Uswisi, Ijumaa.
Bayern wao wametinga nusu fainali kwa maara ya saba katika miaka tisa baada ya kumaliza mechi yao dhidi ya Sevilla kwa matokeo ya bila kufungana lakini wakiwa na magoli mawili kibindoni dhi ya moja la Sevilla katika mechi ya mzunguko wa kwanza.
 
Mazoezi ya kunyanyua vyuma vizito ni moja wapo kati ya mazoezi iitwayo spot resistance training yanayolenga kugusa kundi la misuli ya aina moja kwa kila zoezi moja. Utafiti unaonyesha yakwamba kwa mtu anae enda gym na kufanya mazoezi ya kunyanyua uzito kwa angalau mara 2 ama 3 na dakika zisizo pungua 40 ndani ya wiki, basi mtu huyo anauwezo mkubwa wa kuongeza nguvu na ukubwa wa misuli yake kwa kiwango cha kuridhisha. Hivyo kulingana na utafiti huo ni sawa kusema kwamba ili mtu kupata matokeo mazuri, basi mtu huyo atapaswa kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma vizito angalau mara 3 mpaka 4 kwa wiki.
 
Umekosa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hiyo ni picha ya marehemu EDWARD Moringe Sokoine. Alifariki miaka 34 iliyo pita.
Tulivyo tangaziwa mstarini kuwa amefariki, tulitawanyika huku tukilia.Jioni wengine tukakusanyika na wakubwa tukawa tuna muangalia kwenye kitabu cha vita vya Kagera (Idi Amini) huku tukikumbushwa alivyo kuja kukagua shamba la kijiji-Tenende.
Swali:- Je, ulikuwa umeanza shule?
Nilikuwa darasa la 10
 
Back
Top Bottom