Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Rome, Italia. Kipigo cha Barcelona cha mabao 3-0 ugenini kutoka kwa Roma kimeingia katika orodha ya majanga yaliyoikutaka klabu hiyo ya Catalan.
Barca ilishinda 4-1 nyumbani, lakini wameanga mashindano jambo litakalobaki kwa mashabiki wake kwa muda mrefu.
 
Janga kama hili liliwakuta msimu wa 1984/85 wakati walipoondolewa mashindano na Metz katika mchezo wa kwanza walishinda 4-2 nyumbani katika marudiano walifungwa 4-1.
Pia, msimu wa 1983/83, walifungwa na Manchester United katika mchezo wa kwanza uliochezwa Camp Nou walishinda 2-0, lakini walifungwa katika mchezo wa marudiano 3-0.
 
Real Madrid pia iliwahi kuitoa Barcelona katika nusu fainali na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa tisa wa Ligi ya Mabingwa. Zidane na McManaman walifungwa wakichapa Barcelona mabao 2-0 na katika mchezo wa marudiano uliofanyika Camp Nou timu hizo zilitoka sare 1-1.
 
Back
Top Bottom