Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

D9734A37-88D2-4FAA-AACD-32268C89B0AF.jpeg
 
Mwanasheria mkongwe, Fatma Karume, ameshinda nafasi ya urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Fatma, ambaye licha ya kuwa mwanachama wa TLS kwa muda mrefu, lakini pia ni mtoto wa Rais wa sita wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

Zoezi la kupiga na kuhesabu kura lilianza tangu asubuhi leo Aprili 14, mjini Arusha na likakamilika jioni huku Fatma akiibuka na kura 820 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Wakili Godwin Ngwilimi, aliyepata kura 363.
 
Wagombea wengine wa nafasi ya urais wa TLS walikuwa ni Godwin Mwapongo aliyepata kura 12 na Godfrey Wasonga, aliyepata kura sita.

Fatma ni nani?

Fatma Karume amezaliwa Juni 15, 1969, visiwani Zanzibar,

Ni Mtoto wa rais wa sita wa Zanzibar, Amani Abeid Karume

Ni mjukuu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume.

Ni mwanasheria katika kampuni ya uwakili ya IMMA Advocates

Ni mwanzilishi wa kampuni ya uwakili ya Karume and Co Advocates 2004.
 
Back
Top Bottom