Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

7.KISASI KWA ULIYEACHANA NAYE:


Hapa napo wananasa wengi sana,
yaani utakuta mtu anaachana na mchumba mwezi mmoja nyuma na kwakuwa alimpenda na anataka kumlipizia kisasi basi analazimisha kuingia katika ndoa na mtu mwengine ambaye hajakaa naye hata mwaka kumfahamu.
Hii ni moja ya sababu ya kijinga zaidi kutumia ili kufunga ndoa kwa haraka,
kwani hautakuwa unamkomoa huyo unayetaka umkomoe bali utakuwa unajiingiza katika matatizo wewe mwenyewe
 
NDOA NI KITU KIZURI KATIKA MAISHA PALE INAPOKUWA IMEUNGANISHWA NA UPENDO WA DHATI,
UVUMILIVU NA MALENGO SAWA BAINA YA WANANDOA.

JINSIA, HESHIMA AU UTU WAKO HAUTATAMBULISHWA NA NDOA YA KULAZIMISHA ISIYO NA MALENGO SAHIHI.
KUWA MVUMILIVU NA UVUTE SUBIRA,
KAMA UNASTAHILI KUINGIA KATIKA NDOA UTAINGIA TU LAKINI USILAZIMISHE.
 
[emoji116][emoji116]
Screenshot_2018-04-16-14-30-48-1.jpg
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya mvua inayoendelea kunyesha ili kuepuka majanga.

Akizungumza na MCL Digital leo Aprili 16, 2018; Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi amesema, “Mvua itaendelea kunyesha na hii inatokana na kipindi hiki kuwa na mvua kubwa juu ya wastani.”

Dk Kijazi amesema kwa kawaida Machi na Aprili na zaidi Aprili mvua huwa kubwa juu ya wastani.
 
Ametoa wito kwa wananchi akisema, “Tayari tumeshuhudia maeneo ya bondeni hali ilivyo, kwa hiyo wachukue tahadhari na si wananchi wa bondeni pekee hata maeneo mengine.”

Mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya hali ya hewa, Dk Ladislaus Chang’a amesema, “Mvua inanyesha takriban nchi nzima na itaendelea ndani ya siku mbili. Tunatarajia Jumatano (Aprili 18, 2018) itapungua.”
 
Amesema kama mamlaka ilivyotabiri kuwa kutakuwa na mvua kubwa za wastani, ndivyo imetokea hivyo wananchi wachukue tahadhari.

Dk Chang’a amesema leo Aprili 16, 2018 watafanya tathmini ya hali ilivyo na kutoa taarifa ya saa 24 zijazo.
 
Amesema kama mamlaka ilivyotabiri kuwa kutakuwa na mvua kubwa za wastani, ndivyo imetokea hivyo wananchi wachukue tahadhari.

Dk Chang’a amesema leo Aprili 16, 2018 watafanya tathmini ya hali ilivyo na kutoa taarifa ya saa 24 zijazo.
 
Zaidi ya nyumba 120 zimeharibika vibaya katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa muda wa siku mbili mfululizo.

Kaimu Mkurugenzi Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame akizungumza na MCL Digital leo Jumatatu, Aprili 16 amesema kuwa takwimu hiyo ni ya awali tu ila wanatarajia huenda ikaongezeka zaidi kutokana na maeneo mengi bado hayajafanyiwa uhakiki.
 
Amesema miongoni mwa maeneo ambayo yameathirika na mvua hizo ni pamoja na Amani Kwawazee, Daraja Bovu, Seblen, Mwanakwerekwe, Fuoni pamoja na Kibonde Mzungu.

Amesema mbali ya maeneo hayo lakini pia kuna baadhi ya miundombinu ya barabara nayo imeharibika ikiwamo barabara ya Fuoni pamoja na Mwanakwerekwe ambayo imefungwa kabisa kutokana na kujaa maji maeneo yote na kusindikana vyombo vya moto pamoja na wananchi kushindwa kupita.
 
Back
Top Bottom