Wengi wetu tunapoumwa huwa tunakimbilia kwa madactari kupima na kuandikiwa dawa. wakati mwingine sio ugonjwa wa kutumia dawa, ukitumia dalili zinarudi palepale.
Tafuta kiini cha tatizo, huenda kuna mahali umekosea , inawezekana tatizo lipo katika akili yako, Roho yako, mawazo yako, ikasababisha maumivu ya mwili. huenda kuna kitu ulikula au ulikifanya bila kuwa na imani na hicho kitu au chakula, kikakuletea tatizo.
Watu wengi hufikiri magonjwa ya kurithi hayatibiki. sio kweli. hio ni akili yako inakudanganya. Unao uwezo mkubwa wa kupigana na hio hali kwa kutafuta maarifa ya kutosha kuhusu hilo tatizo.
Unaweza kubadilisha mfumo wa maisha , ukaanza kutumia muda vizuri, unakuwa mwaminifu kazini kwenye ndoa , biashara. unakuwa makini ni vitu gani vinaingia akilini mwako. unalisha nini roho yako, unalisha nini mwili wako. Unasikiliza vitu gani, una mitazamo gani.
Nguvu ya uongo ipo ndani ya mtu . Badili mtazamo wako, badili tabia yako, Acha kulalamika, kulaumu watu, kujilaumu mwenyewe, kusononeka, kujihukumu. shughulikia akili yako, roho yako na mawazo yako pamoja na mwili wako.
Bila kusamehewa dhambi hutaweza kupona ugonjwa ulionao. Anza na Mungu maliza na Mungu. Kumbuka kuwa Dactari anatibu lakini Mungu Anaponya. Neno la Mungu linaponya.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.