Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mambo yanayoweza kukujulisha kuwa umri umeyoyoma.
1. Ukiwa unakula chakula unakuwa mkali ikitokea chakula kimewekwa mafuta mengi ama chumvi nyingi

2. Ukiwa na rafiki zako unapenda kujadiliana nao kuhusiana na mfumuko wa bei, na mfumo mbovu wa utawala

3. Unaanza kujaza friji lako kwa vyakula zaidi kuliko pombe

4. Muziki unaoupenda unausikia ukiwa kwenye lifti ama kwenye gari lako ukienda na kutoka kazini

5. Saa 11 alfajiri ndiyo muda unaoamka, na siyo muda tena unaorudi kulala

6. Unatazama taarifa ya habari hadi utabiri wa hali ya hewa

7. Rafiki zako wanakualika zaidi kwenye vikao vya harusi kuliko mtoko wa kwenda Club

8. Ukienda dukani kununua kitu unakuwa na juhudi sana ya kuomba upunguziwe bei

9. Wewe ndiyo unayekumbuka kuwapigia simu Polisi endapo mtaani kwenu kuna vijana wavuta bangi wanaowasumbua

10. Ndugu zako watu wazima wanajisikia kawaida tu kufanya utani wa kiutu uzima mbele yako

11. Timu yako ya mpira ikifungwa hutaki tena kutaniwa na watu

12. Wanyama uwapendao kama mbwa na paka unawaandalia chakula kwa kanuni za kisayansi badala ya kuwalisha makombo

13. Ukilala kwenye kochi unaamka mgongo unakuuma sana

14. Unaithamini sana ratiba yako ya kulala

15. Ukiwa nyumbani unaanza kutumia muda wako wa ziada kulimalima bustani ya maua ama mbogamboga badala ya kutazama filamu na kuzurura

16. Kila kitu kikinunuliwa nyumbani jambo la kwanza unalouliza, "Umenunua sh. ngapi?"

17. Ukinunua kitu dukani unaangalia sana 'expire date'

18. Unaanza kununua magazeti ya Mwananchi, The Guardian, Daily News, Citizen na Nipashe badala ya magazeti ya udaku

19. Unapata kifungua kinywa kwa wakati

20. Ukiwa baa unanunua bia unazohitaji wewe badala ya kusema "zungusha kama tulivyo"

21. Asilimia 90 ya muda unaoutumia kwenye kompyuta yako unautumia kufanya kazi badala ya kuchati

22. Ukijisikia hamu ya kunywa kilevi unaanza kunywea nyumbani ili kupunguza gharama kabla hujaenda baa

23. Ukimwona rafiki yako ana ujauzito unampongeza sana badala ya kumwuliza, "imekuwaje tena?"

24. Ukienda kutembea mahali unaulizia bei za viwanja

25. Hupendi tena kuwaazimisha marafiki zako magari yako

26. Kwa wanawake utaanza kuona vijana wa kiume wanakukimbia na kwa wanaume utaanza kuona mabinti wanakupenda sana.



Ukiona una robo ya sifa hizi basi huhitaji kupigiwa kengele kukumbushwa kuwa umri ushayoyoma
 
Msichana ni nani? Msichana n Yule dem anaeza toroka kwao usiku aende kwa bf...
Bt haezi enda choo usiku juu kuna giza. [emoji23][emoji28][emoji23][emoji28][emoji15]
Viumbe hivi umri huu huwa ni jasiri sana, mpaka unaweza kumkataa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…